WAKUU katika jimbo la Somalia lilojitenga la Puntland, wanasema walinzi
wa pwani wanajaribu kuikomboa meli iliyotekwa na maharamia zaidi ya
miaka miwli iliyopita.
Meli hiyo, MV Iceberg One, iliyosajiliwa Panama, inazuwiliwa katika
pwani ya Puntland eneo ambalo lina magengi mengi ya maharamia.
Serikali ya Puntland inasema jeshi litaendelea na shughuli hiyo hadi meli na mahabusu wamekombolewa.
Operesheni hiyo imeendelea kwa siku kadha.
Wakuu wanasema maharamia watatu waliuwawa
Jumaane wakati wanajeshi walipokamata mashua ya maharamia iliyokuwa na
shehena ya silaha na vyakula vikipelekwa kwenye meli iliyotekwa.
Vyombo vya habari vya Puntland vinasema
mwanajeshi mmoja ameuwawa; wakuu wanakanusha hayo lakini wanakiri kuwa
watu wao wane wamejeruhiwa.
Puntland inasema mahabusu walikuwa wanazuwiliwa sehemu mbali-mbali lakini sasa wamekusanywa kwenye meli moja.
Mashambulio ya maharamia katika pwani ya Somalia yamepungua sana katika miaka miwili iliyopita.
Wataalamu wanasema sababu ni ushirikiano kati ya
majeshi ya wanamaji ya mataifa mbali-mbali yanayopiga doria katika eneo
hilo na walinzi kuzidishwa ndani ya meli zenyewe.
Hata hivyo, meli kadha na mabaharia wake bado zinazuwiliwa na maharamia.
0 comments:
Post a Comment