IKULU ya rais wa Afrika Kusini
inasema kuwa Nelson Mandela amefanyiwa uperesheni mjini Pretoria,
kutolewa mawe ndani ya kibofu nyongo na anasemekana anaendelea vizuri.
Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini mwenye umri
wa miaka 94, alilazwa hospitali juma moja lilopita kutibiwa mapafu, na
ukaguzi ukaonesha mawe hayo kwenye kibofu.
Katika taarifa iliyotolewa na serikali,
imearifiwa kuwa madaktari waliamua kushughulika na mapafu yake Bwana
Mandela kwanza, kabla ya kufanyiwa upersheni wa Jumamosi.
Wakuu wa Afrika Kusini wamelaumiwa kuwa hawakuwa
wakieleza hali ya Bwana Mandela, ambayo imechochea wasi-wasi zaidi
kuhusu afya yake.
0 comments:
Post a Comment