RAIS wa Misri Mohamed Morsi ameagiza
jeshi nchini humo kuchukua mamlaka ya polisi kuwakamata wale wote
wanaoandamana kupinga kufanyika kwa zoezi la kura ya maoni kupitisha
rasimu ya katiba mpya siku ya Jumamosi, uamuzi ambao serikali inasema
unaanza kutekelezwa mara moja.
Wakati uamuzi huo ukitolewa, maandamano makubwa yamepangwa kufanyika
siku ya Jumanne jijini Cairo nchini Misri, yatakayoongozwa na kundi moja
linalomuunga mkono rais Mohammed Morsi na lingine la upinzani.
Upinzani unasema unatumia maandamano hayo kupinga kufanyika kwa kura
ya maoni kupitisha rasimu ya katiba mpya wakati wafuasi wa rais Morsi
wakisema maandamano yao yatakuwa ni ya kumuunga mkono kiongozi wao.
Muungano wa vyama vya kiislamu nchini humo vinasema vinapinga wito wa
upinzani wa kutaka zoezi la kura ya maoni kuahirishwa kwa kile
wanachokidai kuwa huo ndio wakati wa nchi hiyo kupata katiba mpya na ni
sharti zoezi hilo liendelee kama ilivyopangwa.
Upinzani kwa upande wao unaona kuwa katiba hiyo mpya ikipita
itawabagua pamoja na makundi ya wanawake na pia inagandamiza haki za
wakiristo na wanawake.
Wiki iliyiopita, maelfu ya wapinzani waliandamana katika maeneo
mbalimbali nchini humo kumshinikiza rais Mohammed Morsi kuondoa
madaraka aliyojioongezea suala ambalo alisalimu amri na kuyaondoa lakini
akasisitiza kuwa zoezi la kura ya maoni kuhusu katiba mpya litaendelea
kama ilivyopangwa.
Jeshi nchini humo limetangaza kuwa halitaruhusu waandamanaji kuligawa
tena taifa hilo na watatumia mbinu zote kuhakikisha kuwa wanalinda
amani na kuepusha ghasia zilizosababisha watu saba kupoteza maisha na
mamia kujeruhiwa wiki iliyopita.
0 comments:
Post a Comment