RAIS MAHAMA.
CHAMA cha upinzani nchini Ghana
kimepinga matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu wa urais ambayo yalimpa ushindi
rais John Mahama.
Harakati za uchaguzi nchini Ghana
Chama cha upinzani New Patriotic Party, kimedai kutokea wizi wa kura na kusema kitafanya mkutano hapo keshi kuamua hatua watakazochukua.
Ghana imejipa sifa ya kuwa nchi yenye demokrasia thabiti barani Afrika na moja ya nchi zinazokuwa kwa kasi kubwa barani Afrika.
Kwa upande wake rais Mahama aliwataka watu kuheshimiana kufuatia matangazo ya kura ambayo yalimpa ushindi.
Hapakuwa na ripoti zozote za ghasia Jumatatu asubuhi baada ya matangazo ya uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali kutangazwa siku ya Jumapili.
Furaha na nderemo zilijaa punde baada ya matangazo, huku mamia ya watu wakijitokeza kuonyesha furaha yao kwa ushindi wa rais Mahama.
0 comments:
Post a Comment