BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS OBAMA AMUONYA RAIS KAGAME JUU YA KUWASAIDIA WAASI NCHINI DRC.

RAIS Barrack Obama wa Marekani ametoa wito kwa rais wa Rwanda Paul Kagame, kusitisha msaada anaotoa kwa makundi ya waasi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa ikulu ya White House, Rais Obama alifanya mazungumzo ya simu ya Rais Paul Kagame siku ya jumanne, ambapo aliafiki tangazo lake la kujitolea katika harakati za kupatikana kwa amani katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
RAIS KAGAME.
Waasi wa M-23 wapo katika eneo la mashariki mwa Congo licha ya kuwepo kwa wanajeshi wa kutunza amani wa umoja wa mataifa katika eneo hilo.
 ASKARI WA KUNDI LA M23 WAKIWA WANAKOKOTA TOLORO LENYE MABEKI MOJA YA MIJI WALIYOVAMIA DRC.
Ripoti ya hivi majuzi iliyochapishwa na Umoja wa Mataifa iliishutumu serikali ya Rwanda kwa kutoa msaada kwa waasi hao wa Congo, madai ambayo serikali ya Rwanda Imekanusha vikali.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: