BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RC MORO JOEL BENDERA NA MA-CC WAITWA KORTINI, NI MAHAKAMA KUU KITENGO CHA ARDHI.


KWA UFUPI
Novemba 21, mwaka huu Mahakama hiyo ilitoa zuio kwa Serikali kubomoa nyumba za wakazi 1,994 na kuwahamisha wafugaji na mifugo yao katika vijiji 50 kwenye bonde hilo, mpaka kesi ya msingi ya madai hayo itakapotajwa.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera.

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Ardhi, Dar es Salaam imewataka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na watendaji wake wanne, kufika mahakamani hapo kujibu shtaka la kukaidi agizo la Mahakama la kutowahamisha wananchi wanaoishi katika Bonde la Mto Kilombero na Ulanga.
Amri hiyo ya Mahakama ilitolewa juzi na Jaji Atuganile Ngwala ambaye alimtaka Bendera na wenzake hao, kufika mahakamani hapo, Februari 20 mwakani.
Wengine wanaotakiwa kufika mahakamani hapo ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Hassan Masala, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Francis Miti, Ofisa wa Polisi, Aloyce Nindi na Ofisa wa Polisi Ulanga, Abeid Fanje.
Novemba 21, mwaka huu Mahakama hiyo ilitoa zuio kwa Serikali kubomoa nyumba za wakazi 1,994 na kuwahamisha wafugaji na mifugo yao katika vijiji 50 kwenye bonde hilo, mpaka kesi ya msingi ya madai hayo itakapotajwa.
Kesi hiyo namba 212/2012, ilifunguliwa Oktoba 31, mwaka huu na walalamikaji ambao ni Godfrey Luena, Zablon Mkwage, John Masele, Elia Mtupili na wengine 1998 dhidi ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). 
Wakazi hao walipinga kuondolewa katika eneo hilo bila kulipwa fidia.
Hata hivyo, pamoja na zuio hilo la Mahakama, uongozi wa wilaya hizo uliendelea na operesheni ya kuwaondoa wananchi hao ambao jana walirejea katika Mahakama hiyo kuiomba ichukue hatua.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: