MMOJA WA WAZAZI WALIOPOTEZA WATOTO KWA KUPIGWA NA RISASI AKIANGUA KILIO KATIKA TUKIO HILO.
RAIS wa Marekani Barack Obama anaahidi kutumia uwezo wake wote kuzuia
maafa kama yaliyotokea Ijumaa ya mauaji ya wanafunzi 20 na watu wazima
sita kwenye shule moja ya msingi katika mji wa Newtown, huku wakazi wa
eneo hilo wanajiandaa kwa mazishi ya kwanza kufanyika ya waathirika wa
tukio hilo.
Mazishi ya watoto wawili ambao walikufa katika ufyatuaji holela wa
risasi katika mji wa kaskazini mashariki wa Newtown, Connecticut
yanafanyika Jumatatu huku shule katika wilaya hiyo zikiwa bado
zimefungwa.
Rais Obama aliungana na waombolezaji mjini Newtown Jumapili usiku
akiuambia mkusanyiko wa maafa hayo kwamba hawako peke yao katika majonzi
haya na kwamba taifa limeachwa na maswali magumu.
Alielezea kwamba hii ilikuwa mara ya nne katika tukio la ufyatuaji
risasi holela lililohusisha umati wa watu ambalo limetokea tangu
alipoingia madarakani takribani miaka minne iliyopita.
“Hatuwezi kuvumilia jambo kama hili tena. Maafa haya lazima yakomeshwe
na kukomesha hili lazima tufanye mabadiliko.
Tutaambiwa kuwa chanzo cha
ghasia aina hii hazielezeki kwa urahisi na hilo ni kweli.
Hakuna
sheria, hakuna sheria inayoweza kutokomeza majanga duniani na kuzuia
kila hatua ya ghasia kutokea katika jamii yetu. Lakini hilo haliwezi
kuwa kisingizo cha kutokuchukua hatua”.
Awali Rais alikutana kwa faragha na familia za watu waliopoteza wapendwa
wao katika tukio lililotokea kwenye shule ya msingi ya Sandy Hook na
kuwashukuru waokozi waliojitokeza kutoa msaada katika maafa hayo.
0 comments:
Post a Comment