KWA UFUPI
Alisisitiza kuwa anaheshimu na kukubaliana na masharti ya SADC kwamba yeye pamoja na Rais wa sasa, Andrei Rajoelina aliyewekwa madarakani na jeshi la nchi hiyo, hawatakiwi kushiriki uchaguzi wa Rais utakaofanyika Mei mwakani.
Mark Ravolamanana.
Rais wa zamani wa Madagaska anayeishi uhamishoni Afrika Kusini, Mark Ravolamanana amesema yupo tayari kurudi nchini humo na kwamba hatashiriki kinyanga’nyiro cha urais katika uchaguzi utakaofanyika Mei 2012 kama ilivyopendekezwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Rais huyo ayefukuzwa mwaka 2009 alisema kuwa, anaheshimu uamuzi wa viongozi wa SADC juu ya kumaliza mgogoro wa muda mrefu nchini Madagaska na kwamba, anataka kurudi nyumbani ili kushiriki katika harakati za kuiendeleza nchi yake.
Alisisitiza kuwa anaheshimu na kukubaliana na masharti ya SADC kwamba yeye pamoja na Rais wa sasa, Andrei Rajoelina aliyewekwa madarakani na jeshi la nchi hiyo, hawatakiwi kushiriki uchaguzi wa Rais utakaofanyika Mei mwakani.
“Ninaheshimu uamuzi wa SADC kwamba tusishiriki katika kinyang’anyiro cha urais na nitafanya hivyo nikipewa nafasi ya kurudi nyumbani. Kwa kweli nataka kurudi nyumbani ili kusaidiana na wananchi katika harakati za kuleta maendeleo,” alisema Ravolamanana na kuongeza:
“Nitakwenda nyumbani kama SADC ilivyopendekeza ili kuleta amani na kuijenga upya nchi yetu ambayo imeharibiwa na mgogoro wa kisiasa na utawala uliodumu kwa muda mrefu sasa.”
Alipoulizwa kwamba akirudi nchi kwake atafanya nini wakati amezuiliwa kugombea urais alisema; “Kabla ya kuwa Rais nilikuwa mfanyabiashara kwa takriban miaka 40 ukiachia mbali miaka kumi ya kujihusisha na siasa, hivyo nikirudi nitaendelea na biashara.”
Awali akimkaribisha kiongozi huyo kuzungumza na waandishi wa habari, mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete alisema katika mkutano wa dharura wa viongozi wa SADC uliofanyika Dar es Salaam Desemba 7 hadi 8, mwaka huu walirejea uamuzi wa jumuia hiyo katika mkutano wa maputo kwamba, Rais Ravolamanana arejeshwe nchini kwake bila mashari yoyote.

0 comments:
Post a Comment