Mama Salma Kikwete akitoa chanjo
kwa mmoja wa watoto kuashiria uzinduzi wa chanjo mpya za “PVC 13 na
Rotarix” kukinga watoto dhidi ya Nimonia na magonjwa ya kuhara.
JAMANI, mnakumbuka mwaka huu mwezi April
tulisumbuka sana na ugonjwa uitwao Rotavirus ?.
Maana ulitikisa kwa kama
wiki mbili, unasikia watoto mara wanne, mara sita wamakufa, ila kukawa
hamna kinachoeleweka, hospitali wanasema hawaujui kama basi hofu tu.
Kujikumbushia soma hizi MLIPUKO WA ROTAVIRUS na UPDATE yake.
Well, kama nilivyosema those daya kulikuwa hamna chanjo hapa nchini, now chanjo imekuja, soma hapo chinikuijua !.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wiki imezindua chanjo mpya zinazolenga
kukinga watoto dhidi ya nimonia na magonjwa ya kuhara yanayo sababishwa
na kirusi cha Rotavirus.
Akizindua chanjo hiyo leo Mke wa rais Mama Salma Kikwete amesema kirusi
cha Rotavirus kinachangia asilimia 18 ya vifo vya watoto vinavyotokana
na kuharisha.
Amesema kuongezeka kwa chanjo hizi hapa nchini kutapunguza vifo vya
watoto vitokanavyo na maradhi haya ili kufikia lengo la mileni namba 4
ifikapo 2015.
0 comments:
Post a Comment