BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIKU 260 ZA GODLESS LEMA NJE YA BUNGE

Kwa ufupi
Kwa mara ya kwanza Lema aligombea ubunge mwaka 2005 kwa tiketi ya chama cha Tanzania Labour (TLP), katika uchaguzi uliojumuisha wagombea kutoka vyama saba vya siasa ambavyo ni CUF, Chadema, TLP, SAU, NLP, UDP na CCM.

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema amezungumzia hukumu ya Mahakama ya Rufani iliyotolewa juzi, huku akieleza kuwa katika kipindi cha siku 260 ambacho hakuwa mbunge.

Aprili 5 mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ilitengua matokeo ya ubunge yaliyompa ushindi mgombea wa Chadema, Godbless Lema, baada ya kuridhika kuwa alitumia lugha ya kashfa na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi huo mwaka 2010, Dk Batilda Burian wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Baada ya kushindwa katika kesi hiyo, Lema alikata rufaa na juzi Mahakama ya Rufani ilimrejesha bungeni zikiwa ni siku 260 tangu alipovuliwa wadhifa huo.

Hukumu hiyo iliyosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Elizabeth Mkwizu, ilimtambua Lema kuwa mbunge halali wa Arusha Mjini na kuwaamuru wajiburufaa, kumlipa Lema gharama za rufaa hiyo.

Alikoanzia Lema.
Kwa mara ya kwanza Lema aligombea ubunge mwaka 2005 kwa tiketi ya chama cha Tanzania Labour (TLP), katika uchaguzi uliojumuisha wagombea kutoka vyama saba vya siasa ambavyo ni CUF, Chadema, TLP, SAU, NLP, UDP na CCM.

Katika uchaguzi huo, Lema alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 40,892 sawa na asilimia (40.2) ambapo Felix Mrema wa CCM, aliibuka mshindi kwa kupata kura 47,361 (46.6).

Mgombea wa Chadema Jeremiah Mpinga alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura  6,074 5.

Baada ya kushindwa katika uchaguzi huo, Lema alirudi tena kwenye kinyang’anyiro hicho katika Uchaguzi Mkuu mwaka  2010 kwa tiketi ya Chadema na kuibuka mshindi kwa kupata kura 56,156, akifuatiwa na Dk Batilda Burian aliyepata  kura 36, 470.

Katika kipindi chake akiwa mbunge, Lema alifanya mambo mbalimbali ndani ya Chadema na nje ya chama hicho.

Baadhi ya mambo aliyoyafanya katika siku 260 ambazo hakuwa mbunge wa Arusha Mjini ni kama yafuatayo;

Juni 3.
Amvaa Mkapa.

Baada ya Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kueleza siri ya mafanikio ya uchumi na siasa ya Serikali yake katika miaka 10 aliyokaa madarakani kuwa ni uwazi na ukweli katika mambo yote hata magumu yaliyoikabili Serikali, Lema aliibuka na kumpinga.


Mkapa alikuwa akizungumza katika mjadala maalumu kuhusu uwekezaji barani Afrika, ulioandaliwa na Taasisi ya Uwezeshaji na Uwekezaji (ICF).

Wakati Mkapa akieleza hayo, Lema aliibuka na kumtupia lawama kutokana na umaskini mkubwa unaowakabili wananchi wa Mtwara, licha ya mkoa huo kuwa na utajiri wa kutisha.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: