BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TAIFA STARS YAITANDIKA ZAMBIA 1-0.


 Mshambuliaji wa Taifa Stars,Hamis Mcha (katikati) akiwachachafya mabeki wa timu ya Zambia katika mchezo wa kirafiki uliomalizika muda mfupi uliopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa stars imeshinda goli 1-0.
 Hamis Mcha (7) akiendelea kuwapa kazi mabeki wa timu ya Zambia.
 Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akiingia kwenye lango la timu ya Taifa Stas,huku beki wa Stars,Aggrey Moris akijiandaa kukabiliana nae.
 Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akijaribu kutaka kumtoka beki wa Taifa stars,Salum Aboubakar wakati wa Mchezo wa Kirafiki uliomalizika muda mfupi uliopita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Taifa stars imeibuka mshindi kwa bao moja lililotiwa kimiani na Mshambuliaji machachari,Mrisho Ngassa mnamo dakika ya 45 ya mchezo. 

Mashabiki wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars wakiwa na nyuso za furaha baada ya Taifa Stars kuibuka mshindi kwa kuifunga goli moja dhidi ya timu ya Zambia.Picha Kwa Hisani ya Michuzi Blog

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: