URUSI imetoa wito kwa Sudan Kusini iwape adhabu wale waliohusika na
kudungua helikopta ya Umoja wa Mataifa hapo Ijumaa na kuwauwa Warusi
wane waliokuwamo humo.
Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Urusi ilisema kuwa uchunguzi unafaaa kufanywa sawasawa.
Umoja wa Mataifa ulisema kuwa helikopta hiyo ilidunguliwa na jeshi la Sudan Kusini katika jimbo la Jonglei.
Waziri wa Habari wa Sudan Kusini, Barnaba Marial
Benjamin, alisema hapo jana kwamba sababu ya tukio hilo haijulikani na
kwamba helikopta hiyo ilikuwa ikiruka katika eneo lenye wapiganaji.
0 comments:
Post a Comment