Viongozin wa upinzani Misri
KIONGOZI wa mashtaka ya umma nchini Misri ameagiza uchunguzi dhidi ya viongozi watatu wakuu wa upinzani.
Watatu hao Mohamed ElBaradei, Amr Mousa na Hamdeen Sabahi walianzisha muungano wa upinzani dhidi ya rais Morsi mwezi uliopita.
Kuna wasi wasi kuwa uchunguzi huo unaweza uhusiano kati ya wafuasi wa Bwana Morsi na wafuasi wa viongozi hao.
Viongozi hao wa Upinzani waliunda muungano wa
Upinzani wa National Salvation Front, ili kushiriki katika maandamano
dhidi ya rais Morsi.
Baadhi ya maandamano hayo yalisababisha ghasia
na machafuko wakati wafuasi hao wa upinzani walipokabiliana na wafuasi
wa rais Morsi.
Wapinzani wakuu wa rais Morsi Rais Morsi.
Mousa na Sabahi walikuwa wagombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mwa mwezi Juni ambao Bwana Morsi alishinda.
Siku ya Alhamisi, waziri anayehusika na masuala
ya bunge Mohammed Mahsoub, alijiuzulu akisema kuwa sera za serikali
zinagongana na imani yake.
Mahsoub, mmoja wa wabunge wa Kiislamu walio na siasa za wastani ni waziri wa pili kujiuzulu wiki hii.
Mwendesha mashtaka mkuu wa umma Talaat Ibrahim aliteuliwa na rais Morsi, mwezi uliopita wakati mtangulizi wake alipofutwa kazi.
Uamuzi huo uliwakasirisha majaji wa mahakama kuu ambao waliona kitendo hicho kama shambulio dhidi ya uhuru wa idara ya mahakama.
0 comments:
Post a Comment