Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar
es Salaam, imetuma timu ya Makachero kuja Zanzibar kuungana na wenzao
wengine wa Polisi Zanzibar katika Upelelezi wa tukio la kushambuliwa kwa
Paroko wa Parokia ya Mpendae Amrose Nkenda (pichani).
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa
makosa ya Jinai Zanzibar ACP Yusuf Ilembo, amesema kuwa timu hiyo ambayo
inaongozwa na Afisa mmoja wa ngazi ya juu (hakumtaja jina) ina jumla
ya Makachero watano waliobobea katika masuala ya upelelezi hapa nchini.
Amesema kuwa nia ya Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, kuituma timu hiyo kuja
hapa Zanzibar, ni kutaka kuengeza nguvu katika tukio hili ambalo
linatazamwa kwa aina tofauti hasa ikizingatiwa kuwa aliyeshambuliwa ni
Kiongozi mkubwa wa dini na limetokea katika kipindi cha siku kuu ya
Krismas.
Amesema Jeshi la Polisi limeamua
tukio hili kupelelezwa kwa pamoja kati ya wenzao wa makao makuu ya
Polisi Dar es salaam na wa hapa Zanzibar ili kuhakikisha kuwa wale wote
waliohusika katika kumshambulia Paroko huyo wanakamatwa.
Hata hivyo kamanda Ilembo amesema
kuwabado Polisi wanaendelea na Upelelezi wa kubaini sababu za
kushambuliwa kwa Paroko huyo bila ya kuibwa kwa kitu chochote kutoka kwa
mshambuliwa.
Amesema kuna uwezekana kuwa
watuhumiwa wameshindwa kuchukua kitu chochote baada ya kubaini kuwa eneo
la tukio lisingekuwa salama kwao kwa vile kulikuwa na walinzi na ni
eneo ambalo ni karibu kabisa na makazi ya viongozi wengine wa dhehebu
hilo.
Akizungumzia siku kuu ya mwisho wa
mwaka 2012 na mwanzoni mwa mwaka 2013, Kamanda Ilembo amewahimiza
wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa
taarifa pale wanapobaini kuwepo kwa wahalifu ili wachukuliwe hatua.
Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa
Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amewatahadharisha
wazazi na walezi kutowaruhusu watoto wadogo kuranda barabarani ama
kwenda katika fukwe za bahari kuogelea pasipo uangalizi wa watu wazima.
Kamanda Aziz amesema kuwa uzoefu
unaonyesha kuwa watoto wengi wamekuwa wakigongwa na magari ama kuzama na
kufa maji katika siku hizi za siku kuu za mwisho wa mwaka kwa kukosa
uwangalizi wa watu wazima.
Aidha amewataka wananchi kutoziacha nyumba zao wazi ama bila ya kuwa na uwangalizi wa kutosha ili kutowapa nafasi kwa wahalifu kupata fursa ya kuw
0 comments:
Post a Comment