Kwa ufupi
“Inaonekana ni kama kauli ya kisiasa zaidi kuliko
uhalisia, kwani zoezi hilo linaendelea katika maeneo mengi ya nchi yetu
na linaweza kuleta athari kubwa hasa kwa wananchi wasiokuwa na uwezo
kifedha, watoto wao watakosa elimu,” alisema Mtatiro.
CHAMA Cha Wananchi (CUF), kimemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuingilia kati tatizo la uandikishaji wa watoto wanaojiunga elimu na darasa la kwanza kutozwa michango.
Julius Mtatiro.
CHAMA Cha Wananchi (CUF), kimemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuingilia kati tatizo la uandikishaji wa watoto wanaojiunga elimu na darasa la kwanza kutozwa michango.
Akitoa taarifa kuhusu maadhimio ya kikao cha
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho,
Julias Mtatiro alisema, watoto wote wenye sifa za kuanza elimu ya
msingi wanapaswa kuandikishwa bila masharti na vikwazo vyovyote.
Hata hivyo Mtatiro alikuwa akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba.
Alisema, kipindi cha mwisho wa mwaka, wazazi wengi
nchini wanakuwa katika harakati za kuwapeleka watoto shuleni ili
wakaandikishwe kujiunga na elimu ya msingi.
Alisema hata hivyo wanakutana na vikwazo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutakiwa kulipa michango inayofikia hata
jumla ya Sh50,000 katika baadhi ya maeneo.
Mtatiro alisema hali hiyo inawakatisha tamaa wazazi wengi na kwamba kuna haja kwa Serikali kuondoa kero hiyo.
Mtatiro alisema hali hiyo inawakatisha tamaa wazazi wengi na kwamba kuna haja kwa Serikali kuondoa kero hiyo.
Alisema Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Stadi, Philipo Mulugo alilitolea tamko suala hilo na kuahidi
kuwachukulia hatua kali wale watakaothubutu kutoza michango hiyo.
“Inaonekana ni kama kauli ya kisiasa zaidi kuliko
uhalisia, kwani zoezi hilo linaendelea katika maeneo mengi ya nchi yetu
na linaweza kuleta athari kubwa hasa kwa wananchi wasiokuwa na uwezo
kifedha, watoto wao watakosa elimu,” alisema Mtatiro.
Pia alisema Baraza Kuu la Uongozi la CUF, limemvua
uanachama Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Somanga Ndumo, wilayani
Kilwa Yusuph Muhani, kutokana na uongozi mbaya.
Mtatiroa alisema kiongozi huyo aliingiza taasisi
ya uhifadhi wa fukwe ya bahari kwa njia ya udanganyifu huku akijua kuwa
inaathiri ustawi wa jamii ya wakazi wa kijiji hicho.
Alisema baraza kuu pia limemteua Hamad Masoud kuwa
Naibu Katibu Mkuu kwa upande wa Zanzibar nafasi iliyoachwa na Ismaili
Jussa Ladhu ambaye aliyeomba kuachia nafasi hiyo ili aweze kuwatumikia
wananchi wa Jimbo la Mji Mkongwe.
0 comments:
Post a Comment