Kwa ufupi
Masinde alisema idadi ya vifo vilivyotokana na
Ukimwi katika wilaya hiyo katika kipindi hicho, vimeongezeka kwa
asilimia mbili ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Mchungaji Amilikile Masapila-Loliondo.
IDADI ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi katika Wilaya
na Mkoa wa Geita, inasemekana imeongezeka katika kipindi cha mwaka
2011/12 kufuatia hatua ya baadhi ya wagonjwa, kuacha kutumia dawa za
kupunguza makali ya virusi baada ya kwenda Loliondo kwa babu na kupata
kikombe cha dawa.
Hali kadhalika kuwapo kwa shughuli za migodi ya
wachimbaji wadogo na uvuvi katika Ziwa Victoria, kumechangia ongezeko la
vifo vya watu kutokana na ugonjwa huo.
Imeelezwa kuwa ongezeko la shughuli za kiuchumi katika maeneo ya madini na uvuvi, ni changamoto kubwa kwa idara ya afya wilayani humo katika kupambana na kasi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi kwa wakazi wa Geita.

Mratibu wa Mpango wa Kudhibiti Ukimwi katika
Wilaya ya Geita, Patrisia Masinde, aliiambia Mwananchi jana kuwa katika
kipindi cha kati ya Januari na Novemba mwaka huu, watu 31 walipoteza
maisha kutokana na ugonjwa huo ambao hadi sasa haujapata tiba.
Alisema watu hao ni sehemu ya watu 131,waliokuwa wamelazwa katika vituo vya afya wakipata huduma.
Alisema watu hao ni sehemu ya watu 131,waliokuwa wamelazwa katika vituo vya afya wakipata huduma.
Masinde alisema idadi ya vifo vilivyotokana na
Ukimwi katika wilaya hiyo katika kipindi hicho, vimeongezeka kwa
asilimia mbili ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Kwa mujibu wa mratibu huyo, katika kipindi hicho mwaka jana, watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo walikuwa 16.
Kwa upande wake, Mratibu wa Ukimwi katika Kitengo
cha Matibabu katika Wilaya ya Geita, Dk.John Mgosha alisema vifo hivyo
vinatokana na baadhi ya wagonjwa waliokwenda kwa Babu wa Loliondo na
kupata kikombe cha dawa, kuacha kutumia vidonge vya kuvumbaza virusi vya
Ukimwi.
Alisema baadhi ya watu hao Loliondo waliamini
kwamba Mchungaji Amilikile Masapila, alikuwa na dawa ya kutibu ugonjwa
wa Ukimwi licha ya kutambua kuwa hakuna dawa iliyothibitishwa na
watalaamu wa afya kutibu ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment