NJAMA ya kushambila mkutano wa wajumbe wakuu wa chama
tawala nchini Afrika Kusini, cha African national Congress ANC,
imetibuliwa.
Msemaji wa polisi nchini humo amethibitisha
tukio hilo, na kusema kuwa washukiwa wanne wenye asili ya kizungu wenya
itikadi za siasa kali wamekamatwa.
Rais
Jacob Zuma, na maafisa wengine wakuu wa serikali na wa chama hicho
wanaohudhuria mkutano huo unaoendelea Mangaung, wamepewa ulinzi mkali.
Viongozi wapya wa chama hicho wanatarajiwa kuchaguliwa na wajumbe hao.
Chama cha ANC, kimekuwa madarakani tangu kumalizika kwa utawala wa wazungu walio wachache mwaka wa 1994.
Msemaji wa polisi Phuti Setati, ameliambia
shirika la habari la Reuters kuwa washukiwa wanne ambao walikuwa
wakipanga jinsi ya kuuweka bomu katika eneo la mkutano huo, unaofanyika
katika chuo kikuu cha Free State iliyoko katika eneo la Mangaung.
Zuma kukabiliana na naibu wake
Mwandishi wa BBC Milton Nkosi, ambaye yuko katika eneo hilo anasema, hali ya ulinzi imeimarisha nje na ndani ya ukumbi wa mkutano huo.
Ameongeza kusema kuwa maafisa wa polisi
wanayakagua magari yote na watu wanaoingia katika ukumbi huo kwa kutumia
vifaa maalum na pia mbwa wa kunusa.
Rais Jacob Zuma aliufungua mkutano huo siku ya Jumapili na anawania muhula wa pili kuwa kiongozi wa chama cha ANC.
Hata hivyo Bwana Zuma, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa naibu wake Kgalema Motlanthe.
Mmoja wa wafanyabiashara tajiri zaidi nchini
Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, amemuunga mkono rais Zuma kwa kuwania
kiti cha naibu kiongozi wa chama hicho.
Bwana Ramaphosa alikuwa miongoni mwa watu
mashuhuri waliochangia pakubwa wakati wa mpito kutoka kwa utawala wa
kizungu hadi kwa utawa wa Afrika walio wengi.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, katika eneo hilo
la Mangaung, ambako chama hicho kiliundwa karibu karne moja iliyopita,
rais Zum,a alisema kuwa Afrika Kusini iko tayari kwa awamu ya pili,
ambayo atahakikisha kuafikiwa na maendeleo ya kijamii na kiuchumu
yatayaokuwa na manufaa kwa raia wa nchi hiyo.
Matokeo ya uchaguzi wa viongozi wakuu wa chama hicho yanatarajiwa baadaye wiki hii.
0 comments:
Post a Comment