Kwa ufupi
NI LAZARO NYALANDU, ADAIWA KUMILIKI KAMPUNI YA KITALII, MWENYEWE AJITETEA WAZIRI KAGASHEKI ADUWAA.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (pichani)
anadaiwa kumiliki kampuni inayojishughulisha na masuala ya utalii
kitendo ambacho kinamwingiza kwenye mgongano wa kimasilahi.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Nyalandu
anamiliki Kampuni ya Nitoke Safaris Ltd jambo ambalo limeelezwa kuwa ni
kinyume na Kanuni za Utumishi wa Umma hasa kwa kuwa yeye ni msimamizi wa
sekta hiyo.
Taarifa kutoka kwa Wakala wa Usajili wa Kampuni na
Leseni (Brela), zinaonyesha kuwa wamiliki wa Kampuni hiyo ni
L.S.Nyalandu na Faraja G. Nyalandu, huku kila mmoja akimiliki asilimia
30 ya hisa.
Kampuni hiyo ilisajiliwa Aprili 24, 2009 na kupewa nambari 70735, wakati huo Nyalandu akiwa Mbunge wa Singida Kaskazini, wadhifa alioupata kuanzia mwaka 2000.
Kampuni hiyo ilisajiliwa Aprili 24, 2009 na kupewa nambari 70735, wakati huo Nyalandu akiwa Mbunge wa Singida Kaskazini, wadhifa alioupata kuanzia mwaka 2000.
Ofisi za kampuni hiyo ziko PPF Complex Suit, namba
24 Barabara ya Mzingo, Arusha na magari ya kampuni hiyo yamekuwa
yakibeba watalii mkoani Arusha.
Alipoulizwa kuhusu madai hayo jana akiwa Mwanza,
Waziri Nyalandu alikiri kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo lakini
akasema tayari alishajitoa.
Katika kujenga hoja ya utetezi wake, Nyalandu
alisema kama ambavyo haipendezi yeye kumiliki kampuni ya utalii akiwa
waziri wa wizara hiyo, haitapendeza pia waziri wa habari kumiliki
gazeti.
“Huwezi kuwa Waziri wa Utalii na ukafanya biashara
ya utalii huko katika kampuni hiyo mie nilishatoka kitambo,” alisema
bila kufafanua zaidi.
Hata hivyo, kumbukumbu za Brela zinaonyesha kuwa
waziri huyo bado ni mmoja wa wanahisa ingawa haijafahamika kama ni
tatizo la Brela kutorekebisha kumbukumbu za jalada lake baada ya kujitoa
au la.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi
Kagasheki alipoulizwa na gazeti hili jana alionyesha kushtushwa na
taarifa hizo na kusema hajui kama Naibu wake anamiliki kampuni ya
utalii.
“Siwezi ku comment (kutoa maoni), chochote juu ya jambo hilo kwa sababu sijui kama ana kampuni ya utalii na pili, ndiyo kwanza nasikia hizo taarifa kutoka kwako (mwandishi),” alisema Kagasheki.
“Siwezi ku comment (kutoa maoni), chochote juu ya jambo hilo kwa sababu sijui kama ana kampuni ya utalii na pili, ndiyo kwanza nasikia hizo taarifa kutoka kwako (mwandishi),” alisema Kagasheki.
Taarifa zilizowakariri baadhi ya mawakala wa
utalii mikoa ya Kilimanjaro na Arusha zilidai kuwa Nyalandu ni mmoja wa
washindani katika biashara hasa ya kwenda mbuga za wanyama
Haijafahamika kama Nyalandu aliwahi kutangaza kuwa
na masilahi na kampuni hiyo au kama aliwahi kuiorodhesha kama moja ya
mali anazomiliki kama Sheria ya Maadili ya Viongozi inavyotaka.
“Siyo tatizo kiongozi kumiliki kampuni, lakini unatakiwa ku-declare interest (kutangaza masilahi) lakini kwa Nyalandu ni tofauti kidogo kwa sababu sasa yuko kwenye sekta hiyo,” alidokeza wakili mmoja.

Wakili huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe
alisema hata kama Nyalandu atakuwa haipi upendeleo kampuni hiyo, lakini
kwa akili ya kawaida, ni rahisi binadamu kuhisi kampuni hiyo itakuwa
ikipewa upendeleo wa aina fulani.
0 comments:
Post a Comment