WAPIGA kura wamejitokeza kwa wingi Jumamosi katika mengi ya
majimbo 10 nchini Misri ambako duru ya kwanza ya upigaji kura ya maoni
ya rasimu ya katiba,huku kukiwa na madai ya udanganyifu mkubwa.
Wakati kukiwa na misururu mikubwa katika vituo vya kupigia kura, tume ya
uchaguzi imerefusha muda wa upigaji kura kwa saa nne jana
Jumamosi.
Vituo vya televisheni nchini Misri vimeonyesha misururu ya wapiga kura
wakiwa bado wanasubiri kupiga kura usiku, bila kujali hali ya baridi
kali.
Watazamaji wa uchaguzi huo wamesema kuwa upigaji kura umechafuliwa na
ukiukaji mkubwa, ikiwa ni pamoja na upigaji kura wa halaiki, ukosefu wa
uangalizi kamili wa majaji pamoja na kufanya ushawishi kinyume na
sheria.
Mpiga kura akiwa na karatasi ya kupigia kura.
Mabadiliko bado
"Aina zote za udanganyifu zilizoonekana katika enzi za rais
aliyeondolewa madarakani Hosni Mubarak zimeonekana tena leo," Hafez Abu
Saada , mwanaharakati maarufu wa kupigania haki za binadamu , amekiambia
kituo cha binafsi cha televisheni cha Dream.
Mubarak aliondolewa kiasi miaka miwili iliyopita.
Mkuu wa tume ya uchaguzi Zaghloul al-Balshi amekana madai hayo kwamba upigaji kura hauangaliwi kwa ukamilifu na majaji.
Watu mjini Alexandria wakijitayarisha kupiga kura
"Tutatathmini malalamiko yote ili kubaini athari yake kwa uhalali wa
mchakato huu," ameuambia mkutano na waandishi habari jana
Jumamosi.
Amesema kuwa matokeo yatatangazwa rasmi baada ya duru ya pili na ya mwisho ya upigaji kura itakayofanyika hapo Desemba 22.
Kura ya maoni yaonesha kuelemea kuidhinishwa
Zoezi la kuhesabu kura limeanza jana Jumamosi baada ya
kumalizika kwa upigaji kura huku matokeo ya awali yakionesha kuelekea
kuidhinishwa kwa kura hiyo ya maoni, vimeripoti vyombo vya habari vya
nchi hiyo.
Chama cha rais Mohammed Mursi cha Udugu wa Kiislamu pamoja na washirika
wao wamefanya kampeni kwa nguvu ili rasimu hiyo ya katiba iidhinishwe,
wakidai kuwa ni muhimu kuharakisha hatua za mpito kutoka utawala wa
kiimla wa Mubarak.
Upande wa upinzani unasema kuwa katiba hiyo, iliyoandikwa na baraza
linalomilikiwa na vyama vinavyoongozwa na makundi ya Kiislamu , inaweza
kukandamiza haki za wanawake na za kisiasa na kuwatenga watu wa makundi
ya wachache.
"Sipendi mfumo wa Kiislamu udhibiti nchi yangu kwa sababu nafahamu kuwa
Mursi ni dikteta, anadhibiti maisha yangu na ya familia yangu.
Napendelea uhuru," Naier al-Guindy, mwenye umri wa miaka 59, ameliambia
shirika la habari la dpa katika kituo cha kupigia kura cha Garden City
katikati ya mji wa Cairo.
Utata katika rasimu
Hinar Sabry, mwenye umri wa miaka 25 , msichana ambaye amevaa hijabu, amesema kuwa atapiga kura ya ndio kuidhinisha katiba hiyo.
"Vifungu ambavyo watu wanafikiri vina utata kwa kweli havina utata
hivyo, wanajaribu tu kuleta mtafaruku juu ya katiba hiyo katika
televisheni, amesema msichana huyo.
Mpiga kura akitumbukiza kura yake mjini Cairo
"Hii inahusu zaidi msimamo wa kisiasa kwa upande wa upinzani. Upinzani
unahitaji madaraka tu, na hawajali juu ya kile katiba inachosema."
Mamia kwa maelfu ya wanajeshi na polisi wamewekwa nje ya vituo vya
kupigia kura ili kulinda usalama.
Mshindi wa nishani ya amani ya Nobel
Mohammed ElBaradei, ambaye anaongoza muungano wa upinzani wa National
Salvation Front , amehimiza kura ya "HAPANA ".
0 comments:
Post a Comment