Kwa ufupi
Dk Kigoda ambaye pia ni Mbunge wa Handeni, alikutana
na changamoto kubwa ya wananchi kumlilia chakula cha msaada ama
kinachoweza kuuzwa kwa bei nafuu vijijini, wakidai wengi wao wanakula
mlo mmoja kwa siku au kukosa kabisa.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amebainisha kuwa, wilaya zaidi ya 45 nchini ziko hoi kwa ukosefu wa chakula, sababu ikielezwa kuwa ni kukithiri kwa ukame.
Waziri huyo amewaonya wafanyabiashara kuwa na utu kwa kuacha kuwaumiza wananchi kwa kupandisha bei ya chakula.
Aina mbalimbali za vyakula.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amebainisha kuwa, wilaya zaidi ya 45 nchini ziko hoi kwa ukosefu wa chakula, sababu ikielezwa kuwa ni kukithiri kwa ukame.
Waziri huyo amewaonya wafanyabiashara kuwa na utu kwa kuacha kuwaumiza wananchi kwa kupandisha bei ya chakula.
Akihutubia wananchi katika vijiji mbalimbali vya
Kata za Kwamsisi, Kwasunga na Kwaluguru, Wilaya ya Handeni, mkoani
Tanga, Dk Kigoda alisema kuwa, wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya kati
ya 45 nchini, zinazokabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula, kutokana na
eneo hilo kukumbwa na ukame mkali, hivyo kusababisha baadhi ya wakazi
wake kula mboga za majani.
Kufuatia upungufu huo wa chakula, kumesababisha
mfumko mkubwa wa bei ya mahindi na unga wa sembe kuwa juu, ambapo,
Handeni gunia moja la kilo 100 za mahindi limefikia kuuzwa kati ya
Sh90,000 hadi Sh100,000, kiwango ambacho hakijawahi kutokea wilayani
humo.
Dk Kigoda ambaye pia ni Mbunge wa Handeni,
alikutana na changamoto kubwa ya wananchi kumlilia chakula cha msaada
ama kinachoweza kuuzwa kwa bei nafuu vijijini, wakidai wengi wao
wanakula mlo mmoja kwa siku au kukosa kabisa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kwamsisi,
Athumani Mwagahazi, alimweleza waziri huyo kuwa, wananchi wengi katika
eneo hilo sasa wanaishi kwa kula maembe ya kuchemsha pamoja na majani ya
mchunga.
Akizungumzia hali hiyo Dk Kigoda aliwaeleza
wananchi hao kwamba, Serikali inatarajia kusambaza chakula
kinachotarajiwa kuuzwa kati ya Sh700 hadi Sh850 kwa Mkoa wa Tanga, ambao
unatarajiwa kuwafikia wananchi wiki hii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Handeni, Hassan Mwachibuzi, alisema kwamba wanatarajia kupata tani 150
za unga wiki hii, utakaouzwa Sh750 na 900 kwa kilo moja vijijini katika
Mkoa wa Tanga.
Mwachibuzi alisema bei hizo zinatofautiana
kutokana na gharama za usafirishaji kutoka Jijini Dar es Salaam na
maeneo ya mkoa huo, akisema kwa wilaya ya Handeni ambayo ndiyo iliyopo
karibu na jiji hilo, kitauzwa na wafanyabiashara kwa bei ya Sh750.
0 comments:
Post a Comment