Kwa ufupi
Hayo yalitokea kwenye sherehe ya kumpongeza mgombea
wa CUF, Jafari Nyimage aliyeshinda udiwani katika uchaguzi uliofanyika
Novemba 28.
Mwenyekiti wa CUF,Profesa Ibrahim Lipumba.
CHAMA cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi,
kimevunja kambi iliyokuwa inategemewa na Chama Cha Mapinduzi ya Kijiji
Cha Mkundi, kata ya Makata baada ya wanachama wote wa tawi hilo
kujiunga CUF.
Wanachama hao wapatao 310 wa kijiji hicho ambacho
kilikuwa kinafahamika kwa jina la utani la Dodoma ikiwa na maana ya
makao makuu ya chama tawala walikabidhi kadi za CCM ili wakabidhiwe za
CUF na Mjumbe wa Baraza la Ushauri Taifa la CUF ambaye pia ni Mbunge wa
Lindi Mjini, Salum Barwany.
Hayo yalitokea kwenye sherehe ya kumpongeza
mgombea wa CUF, Jafari Nyimage aliyeshinda udiwani katika uchaguzi
uliofanyika Novemba 28.
Akikabidhiwa kadi ya CUF baada ya kukabidhi kadi
ya CCM kwa niaba ya wanachama wengine, aliyekuwa Mwenyekiti wa tawi hilo
la CCM, Jafari Masura alisema wameamua kujiunga na CUF kutokana na
matamko ya viongozi wa wilaya wa CCM ambapo alidai kuwa mbunge wa jimbo
hilo alipofanya ziara kwenye kijiji hicho mara baada ya matokeo ya
uchaguzi mdogo aliwafananisha wakazi wa kijiji na mbuzi aliyepotea.
“Kauli ya mbunge wetu aliyoitoa mwezi uliopita ya
kutufananisha na mbuzi aliyepotea na kudai amekuja kuwatafuta kutokana
na kumpatia udiwani mgombea wa CUF ilituudhi hivyo tumeamua kukihama
chama hicho”alisema Masura huku akishangiliwa na umati mkubwa wa
wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya kata hiyo.
Akiwakaribisha wanachama hao wapya waliohamia
kutoa CCM mbele ya wanachama na wapenzi wa chama hicho, Barwan
aliwashukuru kwa kuamua kujiunga na chama na kuahidi kufanya kila
linalowezekana kushirikiana katika harakati za maendeleo.
“Sasa hivi uelewa wa wananchi juu ya mfumo wa
vyama vingi umeongezeka sana kwani miaka ya nyuma ilikuwa vigumu kukuta
umati mkubwa kama huu kwenye mikutano ya nyama vya upinzani na hii
ilitokana propaganda za viongozi wa chama tawala ambao walidai upinzani
ungeweza kusababisha vita,” alisema Barwany.
0 comments:
Post a Comment