JESHI la Polisi mkoani Mara, limewakamata watu 15, akiwemo Diwani wa Kata ya
Mugango, Wandwi Maguru (CCM), kwa tuhuma za mauaji ya kikatili yanayoendelea
kutikisa katika wilaya za Butiama na Musoma Mjini.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma, alisema watu hao wamekamatwa
katika oparesheni kubwa inayoendeshwa na jeshi hilo na wapelelezi maalumu
kutoka makao makuu ya jeshi ambayo inaongozwa na Mkuu wa oparesheni, Saimon
Siro.
Alisema Maguru, alikamatwa jana na wenzake kwa tuhuma za
kushirikiana kuua watu kwa kuwachinja kama kuku na kuondoka na baadhi ya viungo
mbalimbali vya mwili.
Kamanda Mwakyoma, alisema watu wanne miongoni mwa watu
waliokamatwa tayari wameshafikishwa mahakamani ambao wametoa ushirikiano katika
kufanikisha kukamatwa kwa watu wengine kutokana na kujihusisha katika matukio
ya mauaji.
“Bado tunaendelea na kazi ya oparesheni kwa kushirikiana na
Jeshi la Polisi makao makuu na kikosi maalum cha askari kutoka Mkoa wa Mara na
kazi inaendelea vizuri,” alisema Kamanda Mwakyoma.
Siku mbili zilizopita, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said
Mwema, aliiambia MTANZANIA kuwa ametuma kikosi maalum ambacho kimekwenda
kuongeza nguvu za kuwasaka wahusika wa mauaji hayo, ambayo wazi yamesababisha
hofu kubwa kwa wananchi.
IGP Mwema, alisema oparesheni hiyo kubwa inafanyika katika
maeneo mbalimbali, hasa katika wilaya za Butiama na Musoma, huku akisisitiza
kuwa kazi hiyo, imetokana na kukamilika kwa kazi ya ukusanyaji wa taarifa
muhimu ambayo imefanywa na timu ya wataalam wa jeshi hilo.
Kwa msingi huo, IGP Mwema aliwaomba wananchi, viongozi wa
vijiji, mitaa na watu wenye taarifa kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano wa
kutosha ambao utawezesha kukamatwa kwa watuhumiwa wote, ili waweze kufikishwa
katika vyombo vya sheria.
Hivi karibuni kumeibuka matukio ya mauaji ya kikatili mkoani
Mara na watu wakichinjwa kama kuku, jambo ambalo limezua hofu kubwa kwa
wananchi.
CHANZO http://www.mtanzania.co.tz.
JESHI la Polisi mkoani Mara, limewakamata watu 15, akiwemo Diwani wa Kata ya Mugango, Wandwi Maguru (CCM), kwa tuhuma za mauaji ya kikatili yanayoendelea kutikisa katika wilaya za Butiama na Musoma Mjini.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma, alisema watu hao wamekamatwa katika oparesheni kubwa inayoendeshwa na jeshi hilo na wapelelezi maalumu kutoka makao makuu ya jeshi ambayo inaongozwa na Mkuu wa oparesheni, Saimon Siro.
Alisema Maguru, alikamatwa jana na wenzake kwa tuhuma za kushirikiana kuua watu kwa kuwachinja kama kuku na kuondoka na baadhi ya viungo mbalimbali vya mwili.
“Bado tunaendelea na kazi ya oparesheni kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi makao makuu na kikosi maalum cha askari kutoka Mkoa wa Mara na kazi inaendelea vizuri,” alisema Kamanda Mwakyoma.
Siku mbili zilizopita, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, aliiambia MTANZANIA kuwa ametuma kikosi maalum ambacho kimekwenda kuongeza nguvu za kuwasaka wahusika wa mauaji hayo, ambayo wazi yamesababisha hofu kubwa kwa wananchi.
IGP Mwema, alisema oparesheni hiyo kubwa inafanyika katika maeneo mbalimbali, hasa katika wilaya za Butiama na Musoma, huku akisisitiza kuwa kazi hiyo, imetokana na kukamilika kwa kazi ya ukusanyaji wa taarifa muhimu ambayo imefanywa na timu ya wataalam wa jeshi hilo.
Kwa msingi huo, IGP Mwema aliwaomba wananchi, viongozi wa vijiji, mitaa na watu wenye taarifa kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano wa kutosha ambao utawezesha kukamatwa kwa watuhumiwa wote, ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Hivi karibuni kumeibuka matukio ya mauaji ya kikatili mkoani Mara na watu wakichinjwa kama kuku, jambo ambalo limezua hofu kubwa kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment