MWAKA mpya wa 2013 umekaribishwa kwa aina yake duniani kote,wakati
mamilioni ya watu wakimiminika katika bandari ya mjini Sydney nchini
Australia,eneo la sherehe mjini Berlin na mjini London kuangalia
fashifashi.
Pia kulikuwa na tukio lililozoeleka la kuweka tufe la dunia katika uwanja wa Times mjini New York , sherehe ambazo zilichafuliwa na kifo mwaka jana cha Dirk Clark , mshauri maalum wa muziki wa rock ambaye kwa miaka kadha amekuwa akisimamia sherehe hizo katika televisheni moja ya Marekani licha ya kuathirika na ulemavu uliosababishwa na ugonjwa wa kiharusi.
Fashifashi zikirushwa angani kuukaribisha mwaka mpya mjini Berlin.
Mjini Berlin , mamia kwa maelfu ya watu waliokuwa wakifurahia waliunganisha mikono yao katika mitaa iliyojaa watu katika juhudi zao za kutaka kuvunja rekodi ya dunia kwa kucheza midundo ya muziki maarufu wa Gangnam style, uliopigwa na mwanamuziki kutoka Korea ya kusini kwa muziki wa kufoka foka Psy. Gangnam , na wachezaji hao walicheza kwa kufuatia mirindimo ya kuhesabu dakika kuelekea mwaka mpya.
Watu wanaokadiriwa kufikia milioni moja walifurika katika eneo maarufu mjini Berlin la sherehe, ambako wanamuziki wa kundi la Pet Shop Boys walitumbuiza na dakika 11 za kurusha fashifashi angani zilikuwa kivutio kikubwa.
Mitaa kuelekea lango kuu la Brandenburg ilikuwa imefurika watu na ilikuwa ni vigumu mtu kuweza kupita kirahisi hata katika saa kabla ya sherehe hizo. Majira ya usiku wa manane , fashifashi 6,000 zilirushwa angani zikisikika kwa sauti kishindo kikubwa na rangi mbali mbali za kupendeza.
Jiji hilo la Berlin lilisikika sauti za kuripuriwa kwa fashifasi mchana kutwa.
Mwaka waanza Australia
Mwaka ulianzia mjini Sydney , ambako zaidi ya watu milioni moja waliokuwa wakijiburudisha walijazana katika bandari ya mji huo kwa ajili ya kuona tukio maarufu la onyesho la kurushwa kwa fashifashi ambalo linakamilisha sherehe za kuukaribisha mwaka mpya na kisha kusogea upande wa magharibi kuifunika dunia yote.
Fashifashi katika bandari ya mji wa Sydney.
Mwanamuziki nyota wa muziki wa pop, Kylie Minogue aliongoza hesabu ya dakika za mwisho kuelekea mwaka mpya akiliongoza kundi la watu waliokuwapo katika eneo hilo ambapo watayarishaji wa sherehe hizo wanasema zinaweza kuzidi zile zinazofanyika kila mwaka mjini New York , mjini London na Berlin.
Mwanamuziki Kylie Minogue akitumbuiza.
Wafilipino wafukuza bahati mbaya ya mwaka jana
Wafilipino kwa kawaida hufanya kelele nyingi, ikiwa ni pamoja na ufyatuaji wa fashifashi, katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kwa imani kuwa wanaifukuza bahati mbaya ya mwaka uliopita na kuvutia bahati nzuri katika mwaka mpya. Baadhi ya watu wanaosherehekea hufyatua risasi hewani.
Vinywaji wakati wa kuukaribisha mwaka mpya 2013.
kiasi ya watu milioni 100 wanatarajiwa kutembelea maeneo ya ibada katika muda wa siku tatu zijazo.
0 comments:
Post a Comment