Kwa ufupi
VYAMA VYASEMA KWA NAMNA YOYOTE ILE GESI HAIONDOKI MTWARA, VYATAKA PROFESA MUHONGO AONDOLEWE, CCM MTWARA KUKUTANA.
RAIS KIKWETE.
SAKATA la wananchi na baadhi ya wanasiasa kupinga usafirishwaji wa gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, limechukua sura mpya, baada ya vyama vya siasa nchini kuungana na kutumia jukwaa kumpinga Rais Jakaya Kikwete, vikisisitiza kuwa gesi haitaondoka Mtwara.

Vyama hivyo pia, vimemtaka Rais Kikwete kumwondoa
katika wadhifa wake, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo, kwa madai kuwa ametoa kauli ya kuwakejeli wananchi wa mkoa huo.
Vyama hivyo vinapinga gesi asilia itayotarajiwa
kuanza kuvunwa katika Mkoa wa Mtwara, kusafirishwa kwa bomba kwenda
jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa haitawanufaisha.
Hata hivyo, Rais Kikwete katika hotuba yake ya Mwaka Mpya, alisema siyo sahihi kwa wakazi wa Mtwara kuizuia gesi isisafirishwe kwenda Dar es Salaam kwa sababu rasilimali hiyo ni ya Watanzania wote.
Hata hivyo, Rais Kikwete katika hotuba yake ya Mwaka Mpya, alisema siyo sahihi kwa wakazi wa Mtwara kuizuia gesi isisafirishwe kwenda Dar es Salaam kwa sababu rasilimali hiyo ni ya Watanzania wote.
Wakihutubia kwa nyakati tofauti mkutano wa hadhara
uliofanyika katika Viwanja vya Soko Kuu, mjini Mtwara jana jioni,
viongozi wa vyama hivyo walisema kwamba hawako tayari kuona rasilimali
za nchi zikiendelea kusababisha umaskini kwa wananchi, badala ya
kuwakomboa.
“Ukicheka na nyani utavuna mabua, wenzetu kwenye
madini walicheka nao na wamevuna mabua, sisi hatuko tayari.
Tunatambua kuwa mamlaka ya nchi yapo mikononi mwetu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kama Kikwete amesema kwa namna yeyote ile gesi itatoka, basi sisi tunamwambia, kwa namna yeyote ile gesi hatoki,” alisema Mohamedi Salim mjumbe wa umoja huo kutoka NCCR- Mageuzi.

Aliongeza:
“Kwanza, tunataka Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo aondolewe katika wadhifa huo kwa sababu analeta propaganda za kisiasa kwenye masuala nyeti yanayohusu maisha ya watu.”
Kwa pande wake, Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mtwara Mjini, Mustafa Nchia alisema kuwa wataandamana hadi Serikali itakaposikia kilio chao na kwamba kwa kuanzia wanataka Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia, aondolewe mkoani humo akidai aliwatusi wananchi kwa kuwaita wapuuzi.

Katika mkutano huo, makamu mwenyekiti wa umoja
huo, Uledi Abdallah alimpongeza Kamanda wa Polisi mkoani humo, Maria
Nzuki, kwa kuruhusu maandamano hayo na kuwataka wananchi kuondoa woga
katika kusimamia rasilimali zao, mradi wasivunje sheria.
Mikutano hiyo itaendelea kesho katika Viwanja vya Bima na keshokutwa katika Viwanja vya Nkanaledi.
Mikutano hiyo itaendelea kesho katika Viwanja vya Bima na keshokutwa katika Viwanja vya Nkanaledi.
Awali, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo unaojumuisha
vyama vya siasa, Uledi Abdallah aliliambia gazeti hili kuwa, kwa siku
tatu mfululizo wanatarajia kuendesha mikutano mikubwa ya hadhara katika
Viwanja vya Soko Kuu, Bima na Mkanaledi.
Uledi ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,
Wilaya ya Mtwara Mjini alisema: “Januari 13, tutawapokea viongozi wa
NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia, wabunge wote wanne wa chama hiki.”
Kamati ya Siasa ya CCM mkoa kukutana
Wakati mkutano huo wa vyama vya siasa ukifanyika, Kamati Siasa ya CCM Mkoa wa Mtwara, inatarajiwa kukutana kesho ili kujadili mgogoro wa gesi na kutoa msimamo wao.
Wakati mkutano huo wa vyama vya siasa ukifanyika, Kamati Siasa ya CCM Mkoa wa Mtwara, inatarajiwa kukutana kesho ili kujadili mgogoro wa gesi na kutoa msimamo wao.
Kamati hiyo itakutana huku tayari kukiwa na
mgongano baina yao, kutokana na chama hicho Wilaya ya Mtwara Mjini,
sambamba na mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji kuunga mkono wananchi
wa mkoa huo kupinga kusafirishwa kwa gesi hiyo inayovunwa katika Kijiji
cha Msimbati mkoani humo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara, Mohamedi Sinani amethibitisha kufanyika kwa kikao hicho kesho Jumatatu.
0 comments:
Post a Comment