BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KATIBU MKUU WA CCM KINANA AKEMEA KASHFA ZA KIDINI.



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman

 Kinana, amewataka viongozi wa dini nchini kuendesha shughuli za 

imani wanazoziamini kwa kuheshimiana. 


Mbali na kutaka waheshimiane alitaka wote wasiopenda 

kubaguliwa dini na imani  zao wasiwe wepesi wa kukashifu imani 

na dini za watu wengine.

Hayo aliyasema wakati wa maadhimisho ya siku ya Imam Hussein, yaliyofanywa na Dhehebu la Khoja Shia Ithna Asheri Jamaat Arusha.

Maadhimisho hayo hufanyika duniani kote ambapo mkoani Arusha yalifanyika kwenye Msikiti wa Jumuiya hiyo na kuhudhuriwa na viongozi wa madhehemu na viongozi wa chama na serikali.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Kinana alisema, changamoto zinajitokeza sasa za baadhi ya watu kukashifu dini nyingine zinapaswa kukemewa na kupingwa.

Alisema pamoja na yote kujitokeza bado Serikali inaendelea kuwa makini na kuwa macho kwa kuhakikisha inawadhibiti watu wenye nia ya kuangamiza amani ya taifa.

“Dini zote nchini zinapaswa kuendesha shughuli zao kwa kuheshimiana. Msingi ya taifa letu inatutaka tusidharau imani wala itikadi ya mtu mwingine.

“Kama wewe haupendi kubaguliwa kwa dini au imani yako, basi usiwe mwepesi wa kubagua imani au dini ya mtu mwingine,’’ alisema Kinana.

Katibu Mkuu huyo wa CCM, aliwaeleza viongozi hao kwamba kwa muda mrefu sasa amekuwa akikerwa na chokochoko hizo ambazo zina kila dalili ya kuondoa amani iliyopo.

“Nitoe wito kwa Taasisi za dini nchini ziendelee kuhubiri amani kwa kuliombea taifa, ili Watanzania waendelee kujivunia amani iliyoachwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,” alisema Kinana.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisema Serikali ipo macho katika kuhakikisha amani inaendelea kulindwa.

Alisema mbali na kuendelea kulinda amani iliyopo Serikali inatambua mchango mkubwa wa madhehebu ya dini nchini katika kuboresha na huduma za kijamii kwa wananchi.

“Niwaombe viongozi wa dini nchini muendelee kudumisha amani iliyopo, kwani tukiendelea kuona baadhi ya wachache wakiichezea gharama ya kuirudisha ni kubwa.

“Tumepata taarifa za baadhi ya watu kujipenyeza ili wavuruge amani kwa kutumia mgongo wa dini, sisi tumejipanga kuhakikisha kila mwananchi anaishi kwa uhuru wa kuabudu mahali popote,” alisema Kasunga.

Naye, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya Khoja Shia, Gulam Hussen, alibainisha kwamba maadhimisho hayo yanalenda kukumbuka mazuri aliyoyafanya Mtume Mohamad.

“Maadhimisho haya yanatambulika kwa jina la ‘Hussein Day’ yanajenga undugu kufahamiana na kupinga ufisadi unaolinyemelea taifa kwa baadhi ya viongozi wenye tamaa ya kujilimbikizia mali,” alisema Hussein.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: