KWA UFUPI
KAMA ni upepo, basi huu ambao umevuma, yaani kwa sasa ndani ya chama hiki kikuu cha upinzani katika nchi, yaani Chadema, si mzuri.
KAMA ni upepo, basi huu ambao umevuma, yaani kwa sasa ndani ya chama hiki kikuu cha upinzani katika nchi, yaani Chadema, si mzuri.
Upepo huu wa mizozo, misigano mingi baina ya viongozi, wanachama wa chama hiki kwa ngazi mbalimbali inaacha maswali mengi.
Upepo huu wa mizozo, misigano mingi baina ya viongozi, wanachama wa chama hiki kwa ngazi mbalimbali inaacha maswali mengi.
Chadema ni chama imara chenye sera na misingi ambayo imejengwa, ni taasisi ambayo inajiendesha kwa kaulimbiu ya ‘nguvu ya watu,’lakini nguvu hii ambayo imeenezwa kupitia operesheni kama Sangara na sasa huu wa Movement For Change (M4C), sasa ipo majaribuni, inaelekea kuanza kuathiriwa na tatizo moja la kupungua kwa nidhamu na kuoneana aibu kwingi.
Hili, sina shaka ni jambo zito ambalo limesababidha mizozo ya chini chini ndani ya chama hiki ambayo kwa upande wangu kwa hakika inanisikitisha.
Niseme, hizi si dalili njema kuanza kuona mipasuko mingi kutoka karibu kona ya nchi yetu ambako kwa miaka karibu mitatu tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani mwaka 2010, kishindo cha Chadema kimesikika, kinafahamika kwa wananchi wengi wa Tanzania, mijini na vijijini.
Hata hivyo, hiki ni kipimo tosha na muhimu ambacho uongozi wa juu wa chama hiki, chini ya ukamanda shupavu wa Freman Aikael Mbowe na mtendaji wake mkuu, Dk Wilbroad Slaa, hawana budi kujiangalia, hasa wakizingatia ukweli kwamba waswahili husema kwamba ivumayo sana hupasuka.
Kama chama, viongozi wa Chadema hawana budi kujiangalia kwa umakini ni wapi wanapoelekea hasa wanapoona chama ambacho wameweza kukijenga, kikakubalika kwa wananchi wengi mijini na vijijini, sasa kinaanza kuyumba, kuwa na makundi ambayo siamini kwamba ni kwa masilahi au maendeleo ya chama chenyewe.
Kwa ushauri wangu, uongozi wa Mbowe na Dk Slaa hauna budi kujifunza kutoka NCCR- Mageuzi, CUF na hata TLP, ambako mizozo, misuguano imeviacha vyama hivyo vikiwa dhaifu mno, vikionekana kama ambavyo havipo.
Kwa ushauri wangu, inafaa uongozi wa juu wa Chadema ukae chini na kutafakari kwa kina mwakaujao watathibiti vipi nidhamu, kumaliza vipi mizozo na mipasuko yote kama hii ya sasa ndani ya chama chao kabla haijavuka mipaka na kukisambaratisha chama hiki ambacho kilianza kuwa tegemeo kwa wengi katika Tanzania.
Ni wazi kwamba uongozi wa Chadema hauna budi uangalie upya, umakini sana kwa mfano kwamba kufanya vizuri kwao kwa mwaka 2013 ni dalili njema ya kufanya vyema pia mwaka 2014 wakati ule wa uchaguzi wa Serikali za mitaa, muda ambao kisiasa kwa jumla si mbali, bali ni muda wa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Ni kwa muktadha huo, ninawashauri Chadema kwamba mafanikio ambayo yamepatikana hayana budi yalindwe kwa gharama zozote, lakini umakini ni kuweza kuondoa mizizi yote ya ubaya ambayo imeanza kujitokeza na kukiathiri chama hata kule katika ngome zake kama Karatu na kwingineko.
Naambiwa kwamba wakiweza kuzingatia ushauri huu, naamini Chadema itakuwa imara, itaheshimiwa na wengi, ijipambanua kwamba imeweza kutatua matatizo yake kwa mafanikio.
Kinyume chake, huu utakuwa mfano mbaya ambao kwa sasa unakinyemelea chama hiki, ambacho kimeifanya Serikali ya chama tawala, CCM isimame wima, kamwe Chadema msiache jukumu hili !.
0 comments:
Post a Comment