MAJESHI ya Mali yamewafurusha waasi wa Kiislamu kutoka mji muhimu katika
eneo la kati nchini humo,baada ya Ufaransa kuingilia kati jana
Ijumaa Januari 11 mwaka huu kwa mashambulio ya anga na kuzuwia waasi hao kusonga
mbele.
Serikali za mataifa ya magharibi , hususan mkoloni wa zamani wa nchi hiyo ufaransa , imeeleza hali ya tahadhari baada ya muungano wa waasi hao wenye mafungamano na kundi la al-Qaeda kuukamata mji wa Konna siku ya Alhamis Januari 10 mwaka huu ikiwa ni njia ya kuingilia katika mji mkuu Bamako, kilometa 600 kusini mwa nchi hiyo.
Ufaransa haitakaa kimya
Rais Francois Hollande amesema kuwa Ufaransa haitakaa kimya na kuwaacha waasi wakisonga mbele kuelekea upande wa kusini.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande.
"Tunakabiliwa na mashambulizi ambayo yanatishia kuwapo kwa Mali,
Ufaransa haiwezi kukubali hali hii, " Hollande, ambaye hivi karibuni
ameahidi kuwa Ufaransa haitaingilia katika masuala ya mataifa ya Afrika,
amesema katika hotuba yake ya mwaka mpya kwa wanadiplomasia na
waandishi wa habari.Wanamgambo wa kundi la Ansar Dine wakiwa kwenye gari huko Gao kaskazini Mashariki mwa Mali.
Rais huyo amesema kuwa maazimio ya baraza la usalama la umoja wa mataifa, ambayo mwezi Desemba yametoa kibali kwa jeshi la Afrika kuingilia kati mzozo wa Mali, yana maana kuwa Ufaransa inafanya hivyo kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Operesheni ya jeshi la Ufaransa ya kuunga mkono jeshi la serikali ya Mali dhidi ya waasi wa Kiislamu, "itafanyika kwa muda wote itakapohitajika," balozi wa Ufaransa katika umoja wa mataifa , Gerard Araud, ameandika katika barua iliyotumwa kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa, ambayo imepatikana na shirika la habari la Reuters.
Balozi wa Ufaransa katika umoja wa mataifa Gerard Araud.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius amethibitisha kuwa Ufaransa imefanya mashambulio ya anga dhidi ya waasi kuwazuwia kukamata nchi yote ya Mali. Alikataa kufichua taarifa zaidi, kama vile iwapo majeshi ya Ufaransa yako katika ardhi ya Mali.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius.
Kuingilia kati kwa Ufaransa haraka kumebadilisha uwiano wa nguvu za kijeshi, ambapo majeshi ya Mali haraka yaliingia tena katika mji wa Konna, kwa mujibu wa wakaazi wa eneo hilo.
Wanajeshi wa Mali.
Majeshi ya Mali yameurejesha katika udhibiti wake mji wa Konna kwa
msaada wa majeshi ya washirika wetu. Tuko katika mji huo hivi sasa,
"Luteni kanali Diaran Kone ameliambia shirika la habari la Reuters, na
kuongeza kuwa jeshi hilo linafanya operesheni ya safisha safisha
kuwaondoa kabisa wapiganaji wa Kiislamu katika eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment