BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTWARA WATOFAUTIANA NA SERIKALI JUU YA BOMBA LA GESI ASILI.

 Mitambo ya kuchimba mafuta.
Mitambo ya kuchimba mafuta
RAIS KIKWETE.

MVUTANO mkubwa umezuka nchini Tanzania baina ya serikali na wananchi wanaotoka mkoa wa Mtwara ambao  wanapinga hatua ya serikali kuweka bomba litakolotumika kusafirisha gesi kutoka mkoani humo hadi mkoani Dar es Salaam.

Wakati serikali ikiendelea kusisitiza nia ya kuendelea na hatua hiyo  mamia ya wananchi wa mkoa wa Mtwara wakiungwa mkono na wabunge wao wanaitaka serikali kusitisha zoezi hilo na badala yale uendeshwaji wa gesi hiyo ufanyike ndani ya mkoa wa Mtwara  eneo ambalo limegunduliwa kuwa na gesi nyingi nchini humo.

Tayari Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospita Mhongo wamezungumzia sakata hilo na kuwataka wananchi hao kuyaweka kando madai yao kwa maelezo kuwa rasilimali zinazoendelea kugundulika ndani ya nchi zitatumika kwa manufaa ya wananchi wote.

Mvutano kuhusu wapi iendelezwe gesi hiyo umezidi kuchukua sura mpya baada ya hivi sasa kujitokeza viongozi wa kidini na kutangaza kuwa wanaunga mkono madai yaliyotolewa na wananchi wa mkoa wa Mtwara ambao wanasisitiza kuwa wananyang’anywa  rasilimali zao.

Kufuatia hali hiyo  mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amezitolea wito pande zote kuwa na majadiliano ya pamoja na hatimaye kutoa suluhisho litakolosaidia uendelezwaji wa rasilimali hiyo.

Wakati huo huo makundi ya wanaharakati hivi karibuni yalikutana na kujadiliana kwa kina sera mpya iliyotolewa na serikali kuhusu  sekta ya gesi. 


Pamoja na mambo mengine makundi hayo ya wanaharakati yalikosoa na kuipinga sera hiyo wakidai  kuwa imejaa  mapungufu.

Wananchi wa eneo la Mtwara pia wameokosoa sera hiyo kwa madai kuwa hawakushirikishwa wakati wa kuandaliwa kwake.

Baadhi ya wabunge kutoka chama tawala cha CCM, wameunga mkono madai yanayotolewa na wananchi hao na wengine wakisisitiza kuwa wako tayari kuchukuliwa hatua zozote na chama  lakini wataendelea kutetea hoja za wananchi wao.  

CHANZO:http://www.voaswahili.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: