RAIS WA CUBA HUGO CHAVEZ.
Bunge la Venezuela litaanza kikao huku wasiwasi ukizidi ikiwa Rais Hugo Chavez ataweza kuanza muhula wake wa pili wa uongozi au la.
Rais Chavez anauguzwa Cuba baada ya kufanyiwa upasuaji kutoa saratani, na inafikiriwa huenda akawa mgonjwa sana na hataweza kuhudhuria sherehe ya kuapishwa juma lijalo.
Hata hivo makamo wa rais, Nicolas Maduro, alisema Chavez anaweza kuapishwa baadae mbele ya mahakama makuu, na alikataa wito wa upinzani kwamba kufanywe uchaguzi mwengine.
Mwandishi wa BBC, Sarah Grainger, akiwa mjini Caracas, alisema kuwa ufunguzi wa kawaida wa bunge la taifa umekuwa muhimu safari hii kwa sababu ya Chavez kukosekana.
0 comments:
Post a Comment