BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Waasi wa Seleka waonywa dhidi ya ukiukwaji wa haki za watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati


Wapiganaji Waasi wa kundi la Seleka wanaokabiliana na Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
SHIRIKA la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa UNICEF limetoa wito kwa waasi wa Seleka wanaokabiliana na Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kuacha kuwaajiri watoto katika vikosi vyao kutokana na matendo hayo kukiuka haki za watoto.

UNICEF imelalamikia vitendo vya unyanyasaji wa watoto ambao wakati mwingine wamekuwa wakilazimishwa kufanya kazi ngumu na hata kunyanyaswa kingono na vikundi vya wapiganaji hao.
Wakati wito huo ukitolewa, matumaini ya kupata suluhu ya mzozo unaoikumba Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yameendelea kusuasua baada ya waasi wa Selekea kudai hawana taarifa rasmi juu ya mazungumzo ya amani yaliyopangwa kufanyika kati yao na serikali mjini Gabon siku ya jumanne.
Akiongea na Shirika la Habari la Ufaransa AFP, Msemaji wa waasi hao Erick Massi amesema hawana taarifa rasmi juu ya mpango huo wa mazungumzo na anashangazwa na taarifa hizo.
Kauli hiyo ya waasi inakinzana na tamko la Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati ambao walitangaza kuwa wataongoza mazungumzo ya amani kati ya Waasi wa Seleka na Serikali ya Rais Francois Bozize.
Serikali ya Marekani pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameendelea kusisitiza pande hizo mbili kukaa katika meza ya mazungumzo ili kupata suluhu ya mzozo huo ambao unaendelea kuathiri maelfu ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: