Kwa ufupi:
TUNDA la stafeli linatibu magonjwa kadhaa, ikiwamo saratani kwa ubora wa karibu mara 10,000 ya matibabu ya kawaida yanayopatikana kwenye vituo vya afya, utafiti umebaini.
Utafiti huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dawa
cha Purdue nchini Marekani, umeeleza kuwa mbali na kutibu saratani,
tunda hilo pia ni tiba ya matatizo ya msongo na mfadhaiko.
Tunda aina la Stafeli.
RAIS JAKAYA KIKWETE AKIANGALIA TUNDA LA STAKAFELI KATIKA MTI WAKE.
TUNDA la stafeli linatibu magonjwa kadhaa, ikiwamo saratani kwa ubora wa karibu mara 10,000 ya matibabu ya kawaida yanayopatikana kwenye vituo vya afya, utafiti umebaini.
Utafiti huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dawa
cha Purdue nchini Marekani, umeeleza kuwa mbali na kutibu saratani,
tunda hilo pia ni tiba ya matatizo ya msongo na mfadhaiko.
“Maajabu ya stafeli ni kwamba lina uwezo wa
kuangamiza chembehai zenye saratani pasipo kusababisha madhara katika
mwili kama zinavyofanya dawa nyingine za ugonjwa huo au mionzi,” imesema
sehemu ya utafiti huo uliochapishwa kwa mara ya kwanza katika Jarida la
Kemia na Madawa la nchini Marekani, mwaka 2010.
Taasisi ya utafiti wa Saratani ya Nchini Uingereza(NIR) ilifanya utafiti wa kwanza kuhusu maajabu ya stafeli mwaka 1976.
Katika utafiti huo ilibainika kuwa majani, mizizi
na tunda la stafeli, vina uwezo wa kutibu saratani, lakini matokeo ya
utafiti huo hayakutangazwa kwa umma kwa hofu ya kuua viwanda vya dawa za
saratani.
Inaelezwa kuwa kirutubisho kilichopo katika
stafeli kinatumia jina la kibiashara la ‘Triamazon’ na kimepigwa
marufuku kutumika nchini Uingereza na Marekani kutokana na uwezo wake
mkubwa wa kitiba.
Utafiti mwingine uliofanywa na Chuo Kikuu cha
Kikatoliki nchini Korea na kuchapishwa katika jarida la Bidhaa Asilia
ulibaini kuwa stafeli lina uwezo wa kuponya saratani ya tumbo.
Utafiti wa chuo hicho ulienda mbali na kusema kuwa
tunda hilo linaweza kulenga seli za saratani tu, bila kushambulia seli
muhimu za mwili kama ambavyo tiba ya mionzi ifanyavyo.
Tunda la Stafeli lina kirutubisho muhimu kiitwacho
Annona Muricata, ambacho ndicho chenye uwezo wa kupigana na maradhi ya
saratani.
Imeelezwa kuwa stafeli lina uwezo wa kutibu aina 12 za saratani ikiwemo ya matiti, kongosho, mapafu na ya kibofu cha mkojo.
Pamoja na kutibu saratani, kirutubisho hicho
kilichopo katika tunda hilo pia huweza kutibu vimelea, shinikizo la
damu, msongo wa mawazo, matatizo ya mfumo wa fahamu na sukari.
Utafiti huo unaonyesha kuwa kirutubisho
kimegwacho katika tunda hilo kinaweza kwa asilimia kubwa kupambana na
saratani bila kumuacha mgonjwa na madhara kama kusikia kichefuchefu,
kutapika, kupungua uzito na kunyonyoka nywele.
0 comments:
Post a Comment