Nyumba ikiteketea kwa moto mkoani Mtwara hii leo katika vurugu zilizozuka.
Magari yakiwa yanateketea kwa moto mkoani Mtwara.
VURUGU zilizotokea mjini Masasi, Mkoa wa Mtwara wiki
iliyopita, zimesababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni 1.5.
Hasara hiyo
imetokana na mali zilizoharibiwa na wananchi wakati wa vurugu hizo, zikiwamo
nyumba zilizochomwa moto, magari yaliyoteketezwa kwa moto pamoja na pikipiki
zilizoharibiwa.
Taarifa hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.
Hata hivyo, Dk. Nchimbi hakueleza hasara iliyosababishwa na vurugu za mjini Mtwara ni kiasi gani kwa kile alichoeleza kuwa, tathmini halisi haijafanyika.
Dk. Nchimbi ambaye alikuwa na Waziri Mkuu katika mkutano huo, alisema Halmashauri ya Masasi peke yake ili iweze kuanza kazi ipasavyo, inahitaji angalau Sh milioni 700 za kununulia samani na zana nyingine za kufanyia kazi bila kuhusisha magari.
Pamoja na hayo, alifafanua zaidi kuhusu madhara yaliyosababishwa na vurugu hizo za Januari 26, kuwa ni pamoja na vifo vya watu wanne waliopigwa risasi wakati wanamshambulia kwa mapanga askari polisi.
Aliwataja waliouawa kuwa ni Bakari Hamis (30), mkazi wa Masasi, Geofrey Simonje (16), mkazi wa Masasi na wengine wawili ambao bado hawajafahamika majina yao.
Aliyataja magari matano ya serikali yaliyochomwa moto kuwa ni ya kubebea wagonjwa yenye namba za usajili SM 3840, SM 9060.
Mengine ni SM 9721aina ya Issuzu Tiper, STK 8417 Toyota Prado, STK Land Rover na jingine aina ya Toyota Maruti ambalo ni mali ya Ofisa Takwimu wa wilaya hiyo.
Magari matano ambayo ni mali ya watu binafsi yaliyochomwa moto ni T120AQP, mali ya James Kiango, T 120 ABM, mali ya Said Manyoya, T 762 AXC, mali ya Mfaume Mashaka, T 402 UBC, mali ya Mashimu Magwila na T 419 BNG, mali ya Vitus Chigwile.
Mengine matano ambayo ni mali ya Serikali yaliyovunjwa vioo aliyataja kuwa ni DPF 3846 Toyota Land Cruiser ambalo ni la mradi wa ukimwi, DFP 748, mali ya hospitali, DFP 3064, mali ya Idara ya Ukaguzi, SM 2633 la Idara ya Elimu ya msingi na STK 5006 aina ya Land Cruiser ambalo ni mali ya Mahakama.
Magari saba ya watu binafsi yaliyovunjwa vioo ni T 607AHA, Mark 11 mali ya Frank Ndembeka, T 692 BTA, mali ya Thomas Mwailafa.
Mengine ni T 275 BHZ, mali ya polisi F5616, T 852 BWY, mali ya Vincent, T 998 ASS, mali ya polisi F1064, T 931 BTQ, mali ya polisi E 721 na Mark 11 mali ya polisi E 9633 koplo Suleiman.
“Pikipiki zilizoharibiwa ni nne ambazo ni zenye namba TZ 98938, mali ya Fredrick Linga, T 773 BLA, mali ya Hassan Said, T 688 AXH, mali ya Said Nanjona, T 178 AVK, mali ya Mwalimu Swani.
“Nyumba ya Ofisa elimu wa wilaya hiyo ambaye hakumtaja jina pamoja na gari la Mbunge wa Masasi, Mariam Kasembe (CCM) vilichomwa moto.
“Mahakama ya Mwanzo Lisekese na Ofisi ya CCM Wilaya ya Masasi viliteketezwa kwa moto na nyumba binafsi ya askari Lusekelo, ilivunjwa vioo, nyumba ya askari E 4696 koplo Hassani ilichomwa moto na askari polisi Osiah Kibona, alijeruhiwa sehemu za kichwani kwa kukatwa mapanga na amelazwa katika Hospitali ya Ndanda na hali yake ni mbaya.
“Polisi wa kike mwenye namba 5576, Eneck William chumba chake kilivamiwa na kundi la watu na kuchukuliwa vitu vyote vya ndani na polisi G 238 PC Lais Saigirani nyumba yake ilibomolewa yote.
“Polisi E 4696 koplo Hassan Lipemba nyumba yake ilichomwa moto na polisi E 234, Koplo Jonas Mweri nyumba yake ilibomolewa yote,” alisema Dk. Nchimbi.
Uharibifu mwingine aliutaja kuwa ni pamoja na kuvunjwa na kuharibiwa kabisa kwa vifaa vilivyonunuliwa kwa ajili ya ukarabati wa ofisi ya kitengo cha fedha ambavyo ni madirisha ya Aluminiam na vigae vyote.

CHANZO http://www.mtanzania.co.tz
0 comments:
Post a Comment