Mkuu wa polisi mkoani Rift Valley John M'mbijiwe anayedaiwa kuwa na
uhusiano na mtu huyo mlaghai,John Waiganjo ingawa alikana kumfahamu.
MAAFISA watatu waandamizi wa polisi nchini Kenya, wamesimamishwa kazi
kuhusiana na sakata ya mtu mmoja ambaye aliwalaghai watu kuwa yeye ni naibu
kamishna mkuu wa polisi kwa zaidi ya miaka mitano.
Mkuu wa polisi mkoani Rift Valley John M'mbijiwe anayedaiwa kuwa na
uhusiano na mtu huyo mlaghai,John Waiganjo ingawa alikana kumfahamu ni mmoja wa
wale waliofutwa kazi.
Mwenyekiti wa tume ya kuwaajiri
maafisa wa polisi KPSC Johnstone Kavulundi, amesema maafisa hao watatu
wametajwa kuhusika kwa njia moja au nyingine na kashfa hiyo.
Wiki iliyopita, Joshua Waiganjo,
alifikishwa mahakamani, kwa kujifanya afisa mwandamizi wa polisi katika mkoa wa
Rift Valley.
Mshukiwa huyo amekanusha madai
hayo.
Ripoti zinasema kuwa ulaghai huo
ulifichuliwa, wakati aliposafiri kwa ndege ya polisi, kwenda kuchunguza mauaji
wa maafisa 42 wa polisi waliouawa na wezi wa ng'ombe katika bonde la Suguta,
tukio ambalo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya taifa hilo.
Rais Mwai Kibaki ameagiza uchunguzi kamili kuhusiana na tukio hilo.
Kavulundi amesema kuwa mkuu
wa polisi mkoani humo John M'Mbijiwe, afisa mkuu wa kitengo cha polisi cha
kupambana na wezi wa mifugo ASTU Remi Ngugi na afisa mkuu wa polisi wilayani
Njoro Peter Nthiga wamesimamishwa kazi.
Amesema watatu hao huenda
wakahujumu uchunguzi ikiwa wataendelea kusalia madarakani.
Joshua Waiganjo amesemekana
kuwafuta kazi na kuwaajiri maafisa wengine wa polisi katika mkoa wa Rift Valley
wakati huo.
Baada ya kukana mashtaka hayo,
kesi hiyo ilihairishwa ili kumruhusu mshukiwa huyo kutafuta matibabu kutokana
na ugonjwa wa kisukari katika hospitali moja nchini humo.
0 comments:
Post a Comment