BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MKUU PINDA AMPONGEZA BIBI-SHAMBA KWA UCHAPAJI KAZI NZURI ITEKA MKOANI KATAVI.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitaka maelezo zaidi kuhusu aina ya mbegu ya mahindi iliyotumika kutoka kwa Bi. Grace Hokororo ambaye ni Bibishamba wa kata ya Itenka wakati alipokuwa akikagua shamba darasa analolisimamia kwenye kijiji cha Itenka wilayani Mlele, Katavi, jana jioni (Januari 6, 2013). Alifurahia kazi yake na kuahidi kumpatia pikipiki imsaidie kutembelea vijijiji vingine vinne anavyovisimamia.
 Bibishamba wa kata ya Itenka, Bi. Grace Hokororo akimshukuru Waziri Mkuu Mizengo kwa kufanya ukaguzi kwenye shamba darasa analolisimamia analolisimamia katika kijiji cha Itenka jana jioni (Januari 6, 2013) wilayani Mlele, Katavi. Aliahidiwa kupatiwa pikipiki ili imsaidie kutembelea vijijiji vingine vinne anavyovisimamia.
Bibishamba wa kata ya Itenka, Bi. Grace Hokororo akipokea zawadi ya sh. 305,000/-kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambazo zilichangwa papo hapo na watu alioandamana nao ili kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye shamba darasa. Wa pili kulia ni Bw. Joseph Laurent anayesimamiwa na bibishamba huyo ambaye shamba lake lilikaguliwa na Waziri Mkuu katika kijiji cha Itenka jana jioni (Januari 6, 2013) wilayani Mlele, Katavi. Pia aliahidiwa kupatiwa pikipiki ili imsaidie kutembelea vijijiji vingine vinne anavyovisimamia.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: