BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HAKI ZA BINADAMU ZAZOROTA DUNIANI, KENYA, SOMALIA NA NIGERIA ZAPOROMOKA KATIKA HAKI ZA BINADAMU NA DEMOKRASIA.

 Security officers walk away as a man mourns next to the bodies of his wife and daughter, who were gunned down outside their house as they attempted to escape when suspected Orma raiders attacked their village of Kibusu in Kenya, January 10, 2013.
 
Mwaka wa 2012 ulishuhudia kuporomoka kwa demokrasia na haki za binadamu nchini Nigeria, Kenya na Somalia.
Wawakilishi  wa kundi la kutetea haki za binadamu- Human Rights Watch, wanasema  katika ripoti yao ya kila mwaka kwamba wana wasiwasi juu hali nchini Syria, Mali na nchi nyingine za kiarabu. Kundi hilo lenye makao yake New York lilitoa ripoti hiyo Alhamis  katika miji ya London na Johannesburg.


Human Rights Watch linasema maandamano ya umma yaliyotokea katika nchi za kiarabu miaka miwili iliyopita hayakuimarisha  haki  kwa raia. Katika ripoti yake ya kurasa  665 iliyotolewa Alhamis kundi hilo linaelezea hali ya haki za binadamu katika nchi 80 ikiwemo Marekani, huku mzozo wa Syria ukiangazwa zaidi kwenye ripoti hiyo ambapo zaidi ya watu elfu 60 wamepoteza maisha yao.



Tiseke Kasambala mkurugenzi  wa kundi hilo tawi la Afrika anasema hali barani humo nayo inazidi kuleta wasiwasi.  “Mwaka wa 2012 ulishuhudia kuporomoka kwa maendeleo ya kidemokrasia  na haki za binadamu  pamoja na tishio la ugaidi katika nchi za Nigeria,  Somalia na Kenya.”



 Kasambala anasema mzozo unaoendelea Mali, Sudan na Sudan Kusini na vita katika  Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo pamoja na Ethiopia na Eritrea, unahujumu maendeleo yaliyopatikana ya haki za binadamu na kanuni za kisheria katika bara la Afrika.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: