MWANDISHI
WETU JOSEPH MWAISANGO AKITOKA KATIKA HOSPITALI YA CHIMALA BAADA YA KUSHUHUDIA
NA KUPATA HABARI ZA UHAKIKA MAANA TAARIFA YA AWALI ILITOLEWA KUWA WATU
WASIOZIDI 30 WAHOFIWA KUFA KATIKA AJALI SASA TUNAHABARI KAMILI BAADA YA MBEYA
YETU KUFIKA KATIKA TUKIO.
WATU
watano wamepoteza maisha na wengine 130 wamejuruhiwa vibaya huku hali zao
zikiwa mbaya baada ya Lori walilokuwa wakisafiria shambani kuacha njia na
kupinduka katika kijiji cha Mapogolo kata ya Itamboleo Wilayani
Mbarali Mkoani hapa.
Ajali
hiyo imetokea leo saa 1:30 asubuhi ambapo lori hilo ambalo ni mali ya
Mwekezaji wa shamba la Kapunga Rice Project, na kwamba watu hao walikuwa
wakielekea kwenye shamba la mwekezaji huyo lililkuwa limebeba vibarua hao zaidi
ya 200 ambao ni wakazi kitongoji cha Kapunga.
Lori hilo
lenye namba za uasjili T398 BSE Scania Tipa, ambalo lilikuwa likiendeshwa na
dereva aliyejulikana kwa jina Baraka Moreli, lilionekana likiwa katika
mwendo kasi na dereva huyo akiwa na lengo la kutaka kuipita
pikipiki iliyokuwa mbele yake. huku akishangiliwa na vibarua hao ipite
ipite hiyo pikipiki haiwezi kutushinda sisi gari kubwa moja ya majeruhi
alisema. ndipo walipofika kwenye kona dereva lilimshinda gari hilo na kupinduka
Akiwa
Hospitalini hapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye aliweza kufika
hospitalini hapo alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo kutoka
kwa Mkuu wa Wilaya ya ,Mbarali Gullam Hussein Kiffuu, huku akiombwa kupatiwa
msaada wa kuongezewa madaktari, kuongezewa vifaa vya mataibu sambamba na
uwezekano wa kupata damu kwa ajili ya kuwaongezea majeruhi hao alifanikiwa
kuwasiliana na uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Mbeya, hospitali ya Mkoa ili
kuweza kuona namna ya kwenda kuokoa maisha watanzania hao.
Kandoro,
alisema kuwa katika ajali hiyo wanaume wanne wamefariki na mwanamke
mmoja. watatu wametambuliwa
Samweli
Mapugilo mbena 30 mkazi wa Ilembula
Bon Mfupa
27 mkazi wa mapogolo na Edgar Mwakipesile 35 mkazi wa Nonde Mbeya.
Aidha,
Kandoro alisema kuwa idadi ya majeruhi katika ajali hiyo kuwa ni 130
ambapo wanawake ni 40 na wanaume 89 huku idadi ya watoto waliokuwa wameongozana
na wazazi wao haikuweza kufahamika kwa haraka.
Picha
Mbeya yetu na Kamanga
|
0 comments:
Post a Comment