Uchaguzi Mkuu wa Kenya 2013.
MAHAKAMA kuu ya Kenya imesema haina uwezo kisheria kuamua kama wagombea
urais katika uchaguzi ujao nchini humo, Uhuru Kenyatta na mgombea wake
mwenza William Ruto, waendelee kugombea au la.
Viongozi hao wa Muungano wa Jubilee wamepata afueni sasa baada ya Mahakama Kuu sasa kuhamishia kesi hiyo kwenye Mahakama ya Juu.
Mahakama hiyo imesema kwa kuwa tayari Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeshakubali uteuzi wa Kenyatta na Rutto kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao, mahakama hiyo haina mamlaka ya kubadilisha uamuzi wa IEBC.
Mahakama hiyo imesma kwamba inao tu uwezo wa kuchunguza upya uamuzi wa
IEBC kuhusu wagombea wengine lakini si wagombea urais na wagombea wenza
wao.
Uamuzi wa Mahakama Kuu
“Taasisi ambayo
ingekuwa na uwezo wa kikatiba wa kuamua kesi hiyo ni IEBC chini ya
kifungu nambari 88 4 (e) cha Katiba ambacho na sehemu ya 74 ya sheria za
uchaguzi ambacho kinatoa ruhusa kwa Tume ya Uchaguzi kutoa uamuzi juu
ya kesi kama hiyo.
Hivyo basi, ingekuwa tofauti ikiwa Tume ya IEBC
ingeshindwa kutekeleza wajibu wake.”
Mahakama hiyo imesema kwamba wawili hao hawana hatia hadi
watakapohukumiwa katika kesi yao inayowakabili huko The Hague na hakuna
mtu anayeweza kubashiri iwapo wawili hao watapatikana na hatia.
Mahakama hiyo imesema kwamba endapo mahakama ya ICCingewasimamisha
wawili hao kugombea nyadhifa za uongozi, basi hilo lingeliwezekana.
Mahakama hiyo imeamua gharama ya washtakiwa kwenye kesi hiyo ilipwe na
wenye kushtaki.
0 comments:
Post a Comment