BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KOLAMU YA MWANANCHI WIKI HII:GESI MTWARA YAWEZAKANA ISIWANUFAISHE WATANZANIA.

KWA UFUPI:

MJADALA wa sakata la gesi huko Mtwara hauwezi kukoma kirahisi, ni vizuri sasa tukazungumzia suala hili kwa mapana zaidi. Ni vizuri tukajiuliza iwapo gesi hii itawanufaisha si tu wananchi wa Mtwara, bali kama itawanufaisha Watanzania wote.
MJADALA wa sakata la gesi huko Mtwara hauwezi kukoma kirahisi, ni vizuri sasa tukazungumzia suala hili kwa mapana zaidi. 

Ni vizuri tukajiuliza iwapo gesi hii itawanufaisha si tu wananchi wa Mtwara, bali kama itawanufaisha Watanzania wote.
Ni kwa sababu iwapo gesi hiyo itawatajirisha watu wachache, basi tunajidanganya tunapobishana kama gesi hiyo ni mali ya Mtwara au ya taifa zima. 

Inawezekana gesi hiyo ikatajirisha kampuni za kimataifa na matajiri wachache wa ndani badala ya wananchi wote wa Tanzania.
Ndiyo maana ni muhimu kuzungumzia sera yetu ya gesi au mafuta au hata dhahabu. Isijekuwa tunagombania kitu ambacho mwishowe kinaliwa na wajanja wachache na wananchi wanaachwa kwenye mataa. 

Kuna maswali kadha ya kujiuliza. Tunapaswa kujiuliza iwapo gesi tunayochimba itawanufaisha si tu wananchi wa nchi hii, bali na vizazi vyao. 

Kosa kubwa ni kujifikiria sisi bila ya kuwafikiria watakaotufuata.
Wataalamu wanatwambia hii gesi ilichukua mamilioni ya miaka ardhini mpaka kufikia umbo la hivi sasa. 

Ni kosa kubwa maliasili hii ikamalizika katika kizazi kimoja. Wajukuu zetu watakuja kutulaani iwapo hatutawaachia chochote kutokana na utajiri huu. 

Ni kosa kubwa iwapo, tutaimaliza gesi na kisha tukaendelea kutegemea wafadhili, iwapo tutawarithisha wajukuu zetu mashimo matupu.

Wasiwasi mwingine ni jinsi mapato yatokanayo na gesi yatakavyotumiwa. 

Je, tutatumia kuinua maisha ya Watanzania au tutafuja utajiri huu katika mambo ya anasa kwa ajili ya watu wachache?

Wakati tulipobinafsisha mashirika yetu, fedha ziliingizwa katika bajeti na zikatumika katika kulipia mishahara minono, marupurupu na posho za wakubwa na mashangingi yao. 

Swali ni iwapo gesi, mafuta na madini yetu yatatumika kuendeleza nchi au tutabaki Rais wetu akitembelea Ulaya na Marekani akiomba ruzuku. 

Mifano ni Cameroon na Nigeria ambako maliasili haikuleta maendeleo kwa wananchi wa kawaida. Matokeo yake ni vurugu. Sudan Kusini nayo inaelekea huko huko.

Hapa Tanzania tumetunga muswada wa sheria yenye nia ya kuifanya Serikali ifaidike kutokana na gesi, mafuta na madini. Sheria kama hiyo imeundwa katika nchi za jirani. 

Swali ni lile lile, je, Serikali kupata mapato mengi maana yake ni maendeleo ya wananchi au ni mashangingi zaidi kwa ajili ya waheshimiwa ?.

Tunahitaji sheria inayohakikisha kuwa fedha hizo zitatumika kwa manufaa ya umma.

Kule India walipouza mashirika ya umma kulikuwa na sheria iliyosema mapato yatokanayo yatatumika katika kuendeleza mashirika yaliyobaki na si kununulia mashangingi ya waheshimiwa.

Sisi hapa tumefuja fedha tulizopata baada ya kuuza mashirika yetu kwa bei ya kutupwa. Kwa nini basi tusiwe na sheria inayokataza jambo hili angalau lisitokee katika sekta ya gesi, mafuta na madini? Katika nchi za jirani masuali kama haya yanaulizwa. 

Uganda wamegundua mafuta mengi katika maeneo ya Bunyoro Magharibi. Tayari wenyeji wa huko wanaona “watoka mbali” wakiingia kwa wingi. 

Jambo hili limesababisha migogoro na wenyeji wamewashambulia “wageni”.

Wakati huo huo wananchi wa Amuru, Uganda ya Kaskazini walipinga uamuzi wa Serikali kutoa ardhi kubwa kwa kampuni ya Madhvani kwa ajili ya shamba la miwa. 

Ardhi hiyo inasemekana ina mafuta mengi na lengo la mwekezaji huyu ni baadaye kufaidika kutokana na mafuta hayo badala ya kupanua shamba la miwa.

Pia kuna malalamiko kutoka wananchi wa Karamoja wanaofukuzwa kutoka ardhi yao yenye madini mengi. Uganda ina sheria inayosema mwananchi mwenye ardhi yenye madini atapatiwa asilimia tatu ya mapato na asilimia 17 zitakwenda kwa wilaya husika.
Utekelezaji wake una matatizo. Mfano ni pale Omukama (mtawala) wa Bunyoro alipowaandikia wabunge barua akilalamika kuwa ugunduzi wa mafuta umekuwa siri kubwa wakati “raia” wake wanaporwa ardhi yao. 

Hili ni suala la uwazi ambalo nasi tunapaswa tujifunze. Kuhusu ugawanyaji wa mapato wenzetu wa Kenya wanabadili sheria ya mafuta ili kuweka utaratibu maalumu wa kugawa mapato kati ya mwekezaji, Serikali Kuu na Serikali ya Kijiji. 

Wao wamegundua mafuta na gesi. Tayari wenyeji wanadai robo ya mapato yote na ndiyo maana imeonekana ni vizuri kuunda sheria kuhusu jambo hili.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: