|
Moses Mwasubira, ambaye alikuwa mwenezi wa Chadema wilaya ya Mbeya akikabidhiwa kadi ya NCCR |
|
Mmoja
wa kada Chadema, Emanuel Mwangoka (Cash Money), ambaye inadaiwa kuwa
ndiye alikuwa mfadhili Mkuu wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi
(Chadema), akikabidhiwa kadi ya chama kipya, alisema atatumia uwezo wake
wote kama alivyofanya kwa sugu kuhakikisha NCCR-Mageuzi inaibuka na
kung’ara mkoani |
Mjumbe wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda,
|
Mjumbe
wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda, katika tukio la
kuwapokea wanachama wapya 21 waliojunga na chama hicho, wakitokea Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
|
|
Aliyewahi
kuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya na kujiunga na NCCR-Mageuzi ,
Januari 20 mwaka huu Eddo Mwamalala, alisema wanachama hao waliomfuata
ni mtaji mkubwa wa kuhakikisha inakimaliza chadema mkoani hapa.
|
|
CHAMA
cha NCCR-Mageuzi, kimesema taifa limepoteza muelekeo kutokana na
viongozi wake wengi waliopewa dhamana ya kuongoza kushindwa kutimiza
wajibu wao, hali ambayo imesababisha wananchi kuishi katika mkanganyiko
mkubwa.
Hayo
yalisemwa jana, Jijini hapa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu taifa ya chama
hicho, Juju Danda, katika tukio la kuwapokea wanachama wapya 21
waliojunga na chama hicho, wakitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema).
Akizungumza
katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Double J,
mbele ya waandishi wa habari, Danda alisema ili taifa liweze kupiga
hatua za kimaendeleo ni lazima liwe na siasa safi na uongozi
bora.
Alisema kutokana na dhana hiyo kukosekana kwa viongozi waliopewa
dhamana ya kuongoza kumesababisha kuliacha taifa na wananchi wake
wakiishi katika mkanganyiko mkubwa unaotokana na kupanda kwa gharama za
maisha.
“Vyakula vimepanda, kadhalika nauli…. Kwa ujumla gharama za
maisha imepanda sana nahii yote imesababishwa na taifa kukosa watu wa
kufanya siasa safi ambazo zingetuletea viongozi bora” alifafanua Danda.
Alisema
msingi pekee wa taifa kupata maendeleo ni rasilimali watu ambayo
imejengwa kwa kupewa elimu, hivyo kitendo cha serikali ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) kukosa mitaala ya elimu ni inaonesha taifa lilivyokosa
muelekeo.
“Rasilimali watu ni muhimu katika mchakjato wa maendeleo
kuzidi hata hayo madini, lakini umeona kilichotokea juzi pale bungeni….
Mwenyekiti wetu (Jems Mbatia-NCCRA-Mageuzi) alichokieleza na
kilichotokea”.
Aliongeza
kuwa licha ya CCM iliyoiweka serikali madarakani kujipambanua kwa
itikadi ya ujamaa na kujitegemea, lakini serikali hiyo imeshindwa
kuisimamia hivyo kufanya taifa kushindwa kujitegemea na badala yake
limegeuka kuwa ombaomba.
Alisema hali hiyo inajidhihirisha kwenye bajeti
ya serikali, kwani zaidi ya asilimia 40 ya bajeti hiyo inategemea
msaada wa wafadhili jambo linalokinzana na mfumo wa itikadi yake
iliyojiwekea kama malengo wakati ikitafuta dhamana ya kupewa nafasi ya
kuongoza nchi.
Kwa
upande wake mwakilishi wa kundi la wanachama 21 waliohamia ndani ya
NCCR-MAgeuzi, Moses Mwasubira, ambaye alikuwa mwenezi wa Chadema wilaya
ya Mbeya Mjini, alisema wamefikia uamuzi huo kutokana na sababu
mbalimbali.
Miongoni mwa sababu hizo ni kudai kuwa uongozi wa taifa wa
Chadema kushindwa kujenga Demokrasia ya kweli ndani ya chama kwa
kukumbatia ufisadi wa kutumia vibaya ruzuku ya chama na kuwaacha wa
mikoani wakifanya kazi kubwa ya kuchangisha fedha.
Uongozi mbaya wa
Katibu Mkuu wa chama hicho taifa,Dk.Willbroad Slaa na Mwenyekiti wake
Freeman Mbowe, kushindwa kusimamia katiba ya chama hicho katika kutatua
migogoro, badala yake wakitumia na kuamini kuwa kufukuza wanachama tena
kwa majungu ndio suluhisho la kukijenga na kukiimarisha chama.
Lakini
pia walilalamikia chama hicho kujaa utashi wa nguvu ya umma na
kulazimisha maandamano, migomo vitu ambavyo si vya lazima na kwamba
kamwe hiyo si njia sahihi na malengo ya kweli ya kutafuta ukombozi.
Naye
mmoja wa kada Chadema, Emanuel Mwangoka (Cash Money), ambaye inadaiwa
kuwa ndiye alikuwa mfadhili Mkuu wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi (Chadema), akikabidhiwa kadi ya chama kipya, alisema atatumia
uwezo wake wote kama alivyofanya kwa sugu kuhakikisha NCCR-Mageuzi
inaibuka na kung’ara mkoani hapa.
Kwa upande wake aliyewahi kuwa Katibu
wa Chadema Mkoa wa Mbeya na kujiunga na NCCR-Mageuzi , Januari 20 mwaka
huu Eddo Mwamalala, alisema wanachama hao waliomfuata ni mtaji mkubwa wa
kuhakikisha inakimaliza chadema mkoani hapa.
Na Mbeya yetu
|
1 comments:
CCM wanaishambulia chadem, CUF wanaishambulia CDM, sasa na NCCR munaishambulia CDM, hebu wataalamu wa mantiki mtufafanulie, hii inamaananisha nini?
Post a Comment