Wanacha wa chama cha mapinduzi kata ya Ruaha na kata jirani sambamba na vitongiji vyake wakiwa katika matembezi ya mshikamano ikiwa ni maadhimisho ya chama cha mapinduzi kutimiza miaka 36 tangu kuzaliwa kwake, ambapo matembezi hayo yalifanyika katika mji mdogo wa Ruaha ikiwa ni maadhimisho ya mkoa wa Morogoro yaliyoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Innocent Kalogeris leo.
Mfumo huu wa waandamanaji wa kutumia vyombo vya moto hususani pikipiki wengi wao wamekuwa wakivunja sheria za usalama barabara jambo ambalo ni hatari endapo mmoja wapo inaweza kumshinda na kuweza kusababisha ajali isiyo ya lazima, si vibaya wahusika wakachukua hatua kwa wavunjivu wa sheria za usalama barabarani ili iwe fundisho kwa wengine.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris (mwenye fulana ya njano) na viongozi wengine akiwemo Mbunge wa jimbo la Mikumi Abdul Salim Amer kulia wakipokea maandamano hayo.
Mwenyekiti huyo wa mkoa wa Morogoro Kalogeris ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Morogoro kusini akihutubia wananchi waliojitokeza wakati wa maadhimisho hayo ya kutimiza miaka 36 ya CCM.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilosa NassoroUdulele akielezea mafanikio ya chama hicho ndani ya wilaya hiyo.
Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Kidodi Arts Group wakitumbuiza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa KKKT Ruaha wilayani Kilosa.
Sehemu ya wachama na wakereketwa wa chama hicho wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea.
PICHA http://www.jumamtanda.blogspot.com/
Sehemu ya wachama na wakereketwa wa chama hicho wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea.
PICHA http://www.jumamtanda.blogspot.com/
0 comments:
Post a Comment