PADRI
Evarist Mushi (55), aliyeuawa juzi kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana
Zanzibar, anatazamiwa kuzikwa Kitope katika eneo lililotengwa la makaburi ya
mapadri.
Akizungumza
na waandishiwa habari jana, Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Zanzibar,
Augostino Shao, alisema maandalizi ya maziko yanaendelea vizuri.
“Tunatarajia
kuupumzisha mwili wa marehemu Mushi katika makaburi ya Kitope ambako kuna
sehemu maalumu ya kuzikwa mapadri,” alisema.
Marehemu
Mushi atakuwa padri wa tatu kuzikwa eneo hilo mkoani Kaskazini Unguja, ambako
alisema kwa sasa ni mapema kujua viongozi watakaohudhuria maziko.
Akielezea
jinsi alivyopokea taarifa ya kifo cha Padri Mushi, ambaye alikuwa msaidizi wake
mkuu, Askofu Shao alisema alipokea wakati akiendesha ibada ya kawaida ya Jumapili
katika Kanisa la Minara Miwili.
“Nilikuwa
naongoza ibada, lakini wenzangu tayari walikuwa wamepata taarifa ya kifo cha
Padri Mushi.
Nilikuwa naye asubuhi saa 12 tukaagana, naye akaenda kuongoza misa
Mtoni katika Kanisa la Beit-el-Ras,” alisema.
Askofu
Shao alivitaka vyombo vya ulinzi, kufanya kazi za kusaka wahalifu kwani jamii
tayari imeanza kupoteza imani.
Padri
Mushi aliuawa kwa risasi tatu alizopigwa kichwani na watu wasiojulikana juzi
saa moja asubuhi, akienda kanisani kuongoza ibada.
Akiwa
katika gari lake aina ya Toyota Hilux Surf, Padri Mushi alipigwa risasi
kichwani kupitia dirisha la mlango wa kulia.
Mauaji
hayo yalifanyika wakati akikata kona kuingia kanisani, ambako watu hao walikuwa
wakimsubiri wakiwa na usafiri wa Vespa na baada ya kumpiga risasi walikimbia.
Kutokana
na hali hiyo, gari la Padri Mushi lilipoteza mwelekeo na kupamia ukuta wa
nyumba iliyo meta chache kutoka Kanisa la Mtakatifu Theresia, ambako alikuwa
akienda.
0 comments:
Post a Comment