Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam jana na vijana waliokuwa wakishiriki mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), uliokuwa unajadili mada ya ‘Nafasi ya Kijana wa Kitanzania katika Shirikisho la Afrika Mashariki’.
Wakizungumza katika mdahalo huo, baadhi ya vijana hao walisema mfumo wa elimu uliopo nchini unadumaza akili za Watanzania katika soko la ushindani la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akichangia mada hiyo katika mdahalo huo, Makamu wa Rais wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Lucy Izengo, alisema kuwa vijana wengi wameshindwa kutambua fursa zilizopo katika shirikisho hilo kutokana na ufinyu wa elimu inayotolewa kuhusu shirikisho lenyewe.
“Kwanza kabisa vijana bado hawajatambua Jumuiya ya EAC ni nini, hivyo wanapaswa kuelimishwa ili kuifahamu kwa kina ndipo waelezwe fursa zilizopo katika jumuiya hiyo.
“Kwa mfano vijana waliopo vijijini hawajapata ufahamu kuhusu jumuiya hii, hili ni tatizo ambalo bado limeendelea kuitafuna Tanzania kwa kushindwa kuchangamkia fursa zilizopo,” alisema.
Kwa upande wake Nicholaus Haule kutoka chuo cha TIA, alisema vyuo vya Tanzania havimjengi kijana wa Kitanzania kujitegemea.
“Hakuna ujuzi wa kutosha ambao utamwezesha kijana kupata ufahamu wa kutosha katika kuvumbua vitu na kujiajiri, badala yake asilimia kubwa ya vijana wameendelea kutegemea kuajiriwa pekee,” alisema.
Alisema mfumo wa ujamaa na kujitegemea ulijenga hofu kwa Watanzania na kushindwa kujiamini.
“Watanzania wengi hawajiamini, ndio maana unaweza kukutana wana elimu ya kutosha lakini tatizo linakuja katika kujieleza, vivyo hivyo kwa wale ambao wanafanya kazi nje ya nchi ni wachache sana badala yake wengi wanataka kuajiriwa hapa nchini,” alisema.
“Wenzetu Kenya na Uganda, huanza kufundisha lugha kuanzia chekechea ndio maana wanaweza kuizungumza kwa ufasaha kwa sababu Tanzania huanzia darasa la tatu tena kwa somo la Kiingereza pekee,” alisema.
0 comments:
Post a Comment