BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA YAKALIA BAO 1-0 DHIDI YA LIBOLO FC LIGI YA MABINGWA AFRIKA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM


KWA UFUPI
Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu alikubali kipigo hicho na kusema: “Haya ni matokeo ya kawaida, wamepata bao moja ambalo wameona ni muhimu kwao.”
Mshambuliaji wa Simba Mrisho Ngassa (kushoto), akitafuta mbinu ya kuwatoka mabeki wa timu ya Libolo ya Angola katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja Taifa, Dar es Salaam jana. Simba ililala bao 1-0. Picha na Michael Matemanga. 
WAWAKILISHI wa Tanzania michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Simba jana waliwainamisha chini vichwa mashabiki wao baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbali na huzuni ya kipigo, pia mashabiki wa Simba hawakufurahishwa na kiwango dhaifu kilichoonyesha na wachezaji wao.
Kocha Patrick Liewig naye alikiri Simba kucheza ovyo. Matokeo hayo yanawaweka kwenye wakati mgumu kusonga mbele katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo.
Libolo walitawala sehemu kubwa ya mchezo na dhahiri walionekana kama vile walikuwa wanacheza uwanja wa nyumbani na siyo ugenini.
Safu ya kiungo ya Simba chini ya Mwinyi Kazimoto, Amri Kihemba na Mussa Mudde walishindwa kutibua mashambulizi ya Libolo.
Hali hiyo ilikaribisha mashambulizi mengi langoni kwao, lakini pia wakishindwa kuwatengenezea mipira washambuliaji wao ili kulitia misukosuko lango la Libolo.
Washambuliaji wa Simba wakiongozwa na Mrisho Ngassa na Haruna Moshi walishindwa kufanya shambulizi la maana kipindi chote cha kwanza.
Wafungaji hao walionekana kutafuta zaidi mipira iliyokuwa inamilikiwa na Libolo kuliko kutengenezewa nafasi za kufunga.
Mashabiki wengi wa Simba, walilipuka kelele za kupinga mabadiliko ya kupumzishwa Boban na kuingizwa Hamis Kinje dakika ya 80.
Nusu ya kipindi cha kwanza ilitawaliwa na Libolo waliokuwa wakishangiliwa muda wote wa mchezo na mashabiki wanaodhaniwa kuwa wa Yanga.
Kelele hizo za kushangiliwa ziliwatia nguvu kiasi cha kuumiliki na kuucheza mpira walivyotaka na kuwaacha mashabiki wa Simba wakishangaa.
Simba walizinduka muda wa robo tatu ya mchezo kwa mashambulizi makali mawili kutoka kwa Boban na Kihemba ambayo mikwaju yao ilikosa shabaha na kutoka nje.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: