KWA UFUPI
Aliwataka polisi kuwa na mbinu za kukabiliana na matukio kwa kutosababisha madhara kwa raia na kwamba, wawapende raia na kuwaona kama ni sehemu yao wakati wote. Pia, alikemea kwa nguvu malalamiko yatolewayo na raia kuwa, wamekuwa wakipigwa hata pale wanapofanyiwa mahojiano ya kawaida, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu na kanuni za polisi.
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewageuka polisi na kuwataka kuangalia jinsi wanavyowaumiza askari wa vyeo vya chini, kutokana na amri zinatolewa na wakubwa wao, nyingi zikiwa za uvunjaji haki za binadamu.
Pia, Pinda alionya fikra potofu ambazo zimejengwa miongoni mwa polisi katika kufanya maovu na kukimbilia kuunda tume, ambazo nyingi hazina majibu ya kutosha kwa wananchi.
Alisema matokeo yake zimekuwa ziitoa taarifa zenye utata, kwani ni vigumu kujichunguza wenyewe huku wakiwa watuhumiwa.
Alitoa kauli hiyo wakati akifunga mkutano wa maofisa na makamanda wa polisi nchini.
Kauli ya Pinda juzi ilionekana kutofautina na ile iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete, ambaye wakati wa ufunguzi alionekana kuwasifia polisi kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka wakaze uzi hasa nyakati za maandamano.
Juzi, Pinda alisema moja ya vitu ambavyo vinaiondolea sifa polisi, ni ukiukaji haki za binadamu na masuala ya rushwa ambayo yanaonekana kukithiri.
“Tatizo lingine ni jinsi ambavyo mmekuwa mkiwashurutisha askari wa vyeo vya chini na kuwaadhibu katika amri ambazo mmetoa ninyi, hilo jambo siyo zuri hata kidogo, ufike wakati mwangalie basi kama mnaweza kubadilisha mwelekeo ili wanaotoa amri za uvunjaji haki za binadamu washughulikiwe kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Aliwataka polisi kuwa na mbinu za kukabiliana na matukio kwa kutosababisha madhara kwa raia na kwamba, wawapende raia na kuwaona kama ni sehemu yao wakati wote.
Pia, alikemea kwa nguvu malalamiko yatolewayo na raia kuwa, wamekuwa wakipigwa hata pale wanapofanyiwa mahojiano ya kawaida, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu na kanuni za polisi.
Awali, Mkuu wa Polisi Tanzania, Said Mwema alimweleza Pinda kuwa mkutano huo ulikuwa wa mafanikio makubwa, uliweka maazimio makubwa manne.
Mwema aliyataka maazimio hayo kuwa, ni kujenga uwezo wa askari kupambana na vitendo viovu, kuimarisha misimamo ya askari katika nidhamu na uadilifu, kuimarisha ustawi wa jamii na wanaofanya vizuri watazawadiwa.
0 comments:
Post a Comment