Kwa ufupi
Mkurugen-zi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert
Manumba amezung-umzia ugonjwa wake ambao ulisababisha kutojitambua kwa
siku 42 na kwamba sasa anaendelea vizuri.
Mwananchi Johannesburg.
Mkurugen-zi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba amezung-umzia ugonjwa wake ambao ulisababisha kutojitambua kwa siku 42 na kwamba sasa anaendelea vizuri.
http://www.mwananchi.co.tz
DCI MANUMBA.
Mwananchi Johannesburg.
Mkurugen-zi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba amezung-umzia ugonjwa wake ambao ulisababisha kutojitambua kwa siku 42 na kwamba sasa anaendelea vizuri.
Kwa sasa Manumba ambaye amelazwa nchini Afrika
Kusini kwa matibabu, anaendelea vizuri na sasa anafanya mazoezi mepesi
ya kusimama na kutembea kama sehemu ya matibabu yake.
“Kwa sasa ninashukuru naendelea vizuri,
nina-washukuru madaktari wa hapa ambao wamejitahidi maana ni kama watu
wal-ishakata tamaa kwamba siwezi kupona,” alisema Manumba alipozungumza
na Mwananchi katika Hos-pitali ya Millpark alikolazwa jijini
Johannesburg.
Alisema tatizo kubwa lili-lokuwa likimkabili ni
ugon-jwa wa malaria kwani ali-popimwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili alikutwa na wadudu wa ugonjwa huo 500.
“Yaani huwezi kuamini, nilikuwa na wadudu 500
lakini nilikuwa naendelea na kazi tu kama kawaida, sasa tiba ya malaria
ndiyo ilisababisha kuibuka kwa magonjwa mengine lukuki ambayo
yalisababisha nisiji-tambue kwa siku 42,” alise-ma Manumba.
Manumba anasema ni kwa mkono wa Mungu amepa-ta nafuu kubwa baada ya juhudi kubwa za madaktari katika kupigania uhai wake.
Alipelekwa Afrika Kusini Januari 23, mwaka huu baa-da ya kupata nafuu kidogo.
Alisema anawashukuru madaktari wote walio-hangaika
usiku na mchana katika hospitali alizolazwa kuanzia Muhimbili na Aga
Khan, jijini Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwa ndege maalumu hadi
Johan-nesburg, Afrika Kusini.
Kadhalika alilimshukuru Rais Jakaya Kikwete
kwam-ba ndiye alisaidia kuhara-kishwa kwa mchakato wa kuhamishiwa jijini
hapa kwa ajili ya matibabu zaidi ambayo yamemrejeshea uzima ambao
tayari ulikuwa kama umepotea.
Kwa kweli sasa kama mnavyoniona sijambo sana.
Nimeanza kufanya mazoezi. Sijambo kwa kweli inga-wa bado niko hospitalini naendelea na matibabu,” alisema Manumba.
Nimeanza kufanya mazoezi. Sijambo kwa kweli inga-wa bado niko hospitalini naendelea na matibabu,” alisema Manumba.
Wakati huohuo, Mwe-nyekiti wa Jukwaa la Waha-riri
Tanzania (TEF), Absa-lom Kibanda, amezungum-zia tukio la kuvamiwa kwake
huku akiweka bayana kuwa, watesi wake walikusudia kumtoa uhai.
“Kwa muda mrefu nili-kuwa nimedokezwa na rafiki
yangu mmoja kuwa ninapokwenda nyumbani niwe mwangalifu kuanga-lia nani
hasa yuko nyuma yangu usiku, lakini kwa siku ile sikuona kama kuna watu
walikuwa wakinifuatilia,” alisema katika mahojiano na gazeti Mwananchi.
0 comments:
Post a Comment