WAANGALIZI WA KIMATAIFA WALISEMA UCHAGUZI WA KENYA ULIKUWA WA AMANI NA MATOKEO YAKE YANAAMINIKA.
Rais mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Waziri mkuu anayeondoka Raila Odinga akiwahutubia wafuasi wake Nairobi, Machi 16, 2013.
Mapema Jumamosi polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kutawanya waandamanaji waliokusanyika nje ya mahakama kuu ya Kenya, kuunga mkono waziri mkuu anayeondoka Raila Odinga.
Muungano wa chama chake -CORD unasema una imani Bw. Odinga atashinda kesi hiyo. Bw. Odinga alikataa kukubali matokeo ya uchaguzi huo akidai kulikuwa na kasoro wakati wa kuhesabu kura.
Hapo awali Odinga alikuwa ameahidi kama wagombea urais wenzake ,kuwa ataheshimu matokeo ya kiti cha urais.
Tume huru ya uchaguzi Kenya, ilimtangaza Bw. Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa urais kwa kuzoa asili mia 50.07 ya kura na hivyo kuepuka uchaguzi wa marudio.
Waangalizi wa kimataifa na wale wa ndani ya nchi walisema uchaguzi huo ulifanyika kwa njia ya amani na kwamba matokeo yake yanaaminika.
0 comments:
Post a Comment