Taarifa iliyotolewa na kuthibitishwa na Msemaji wa Polisi
Advera Senso, imesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Familia ya Marehemu
tayari imefanikisha kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda Kijijini kwao Mwera
mkoani Tanga, kwa ajili ya Mazishi.
Senso
alisema Kufuatia msiba huo Jeshi la Polisi nchini limepata pengo kubwa kwa
kuondokewa na kamishina huyo kwa kuwa alikuwa mtendaji hodari hali iliyopelekea
kutunukiwa nishani ya utumishi wa muda mrefu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete.
Alisema
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema amezipokea taarifa za kifo hicho
kwa huzuni hasa ukizingatia hivi sasa Askari mmoja anahudumia watu takribani
1300 hadi 1500 hivyo kufariki kwa Ofisa, Mkaguzi au Askari mmoja ni pengo kubwa
kwa Jeshi la Polisi na Watanzania hasa katika nyanja ya usalama na ameitumia
familia ya marehemu salamu za rambirambi.
ACP Kimea alijiunga na Jeshi la Polisi Mwaka 1985 na kupandishwa
vyeo mbalimbali hadi kufikia Cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi ambapo mpaka
mauti yanamkuta alikuwa mkuu wa Kitengo cha Mipango ya Raslimaliwatu (Human
Resource and Planning) Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na nafasi nyingine
alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mkuu wa Upelelezi wilayani Misungwi, Mkuu
wa Polisi wilayani Misungwi na Geita pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Polisi Mkoani
Morogoro.
0 comments:
Post a Comment