BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI MORO SC YAIKARIBISHA YANGA SC KATIKA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA UWANJA WA JAMHURI MOROGORO LEO.

KIKOSI CHA YANGA SC.
KIKOSI CHA POLISI MORO SC.
TIMU ya soka ya Polisi Moro SC inapambana na Yanga SC katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara katika uwanja wa jamhuri jioni ya leo.

Mchezo huo unatarajia kuwa mkali na vuta ni kuvute kutokana na kila timu kutaka kupata pointi tatu muhimu huku Yanga SC ikihitaji pointi hizo ili kujiimarisha katika mbio za kujikita kilele baada ya kuwa na pointi 48 huku ikiongoza ligi kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya Azam SC yenye pointi 40 anayeshika nafasi ya pili.

Kwa upande wa vijana wa Mohamed Adolf Richard Polisi Moro SC yenyewe inahitaji kupata ushindi wa kila hali na mali ili kujinasua na janga la kushuka daraja ambapo kati ya mechi tano zilizosalia watahitaji kushinda zote ili kumaliza ligi na pointi 32 ambapo kwa sasa wanapointi 17.

Ushindi kwa Polisi Moro SC dhidi ya Yanga SC katika mchezo wa leo utasaidia kuongeza morali kwa michezo ijayo ya timu hiyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: