Rais wa Marekani Barack Obama alipokutana na
viongozi wa Afrika huko White House viongozi hao kutoka kushoto ni rais
Macky Sall wa Senegal, rais Joyce Banda wa Malawi, Obama, rais Ernest
Bai Koroma wa Sierra Leone na waziri mkuu wa Cape Verde Jose Maria
Pereira.
RAIS wa Marekani Barack Obama alikuwa mwenyeji wa viongozi wa Cape
Verde, Malawi, Senegal na Sierra Leone katika White house alhamisi ,
akisifu hatua kubwa za uchumi nchi zao zimefanya pamoja na maendeleo
ya kuimarisha utawala wa kidemokrasia.
Bw.Obama alisema kwamba wageni wake wote wa Afrika walikuwa na
changamoto zao za kisiasa nyumbani, ikiwa ni pamoja na vita vya wenyewe
kwa wenyewe Sierra Leone, mzozo wa hivi karibuni wa kikatiba huko
Malawi na mzozo wa kisiasa huko senegal , hata hivyo nchi hizo
zimefanikiwa kudumisha utulivu na kupata maendeleo ya kiuchumi.
Viongozi katika mkutano huo walikuwa ni Ernest Koroma wa SierraLeone ,
rais wa Senegal Macky Sall , waziri mkuu wa Cape Verde Jose Maria
Pereira na rais wa Malawi Joyce Banda.
0 comments:
Post a Comment