BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA SC YAZINDUKA, YAICHAPA COASTAL UNION KWA BAO 2-1 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

 
 Mrisho Ngassa akiifungia Simba SC bao la kwanza leo. Kipa Shaaban Kado amekwishapotea mabode kulia, langoni yupo beki Philip Mugenzi, ambaye hakuwa na la kufanya.

Wachezaji wa Simba, Abdallah Seseme, Amri Kiemba na Mrisho Ngassa wakimpongeza Haruna Chanongo (6) kufunga bao la pili katika mchezo wa leo.
Picha kwa hisani ya Bin Zuber Blog.

SIMBA 2-1 COASTAL.
Simba SC imerejesha heshima kwa mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara katika mchezo uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Ushindi huo  kwa Simba SC umepatikana miguuni mwa wachezaji Mrisha Ngassa aliyefunga bao katika dakika ya dakika ya 45 baada ya kuvunja mtego wa kuotea wa Coastal na kukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao la kwanza.

Katika dakika ya dakika mbili baadaye mchezaji chipukizi Haruna Chanongo anaipatia Simba bao la pili baada ya kugongeana vyema na Mrisha Ngassa na kuandika bao hilo wakati bao la Coastal lilipatikana katika dakika ya 49 kwa mchezaji Razack Khalfan kuipatia timu yake bao hilo.

KIKOSI CHA SIMBA SC: 
Abel Dhaira, Nassor Masoud 'Chollo', Miraji Adam, Hassan Khatib, Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Rashid Ismail, Abdalah Seseme, Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa.
KIKOSI CHA COASTAL UNION
 Shaaban Kado, Hamad Juma, Abdi Banda, Philip Mugenzi, Mbwana Kibacha, Razakh Khalfan, Mohammed Sudi, Suleiman Kassim 'selembe', Mahundi, Danny Lyanga na Gabriel Barbosa. 
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: